Vitisho Vya Kutekwa, Kuuawa Na Kupotezwa Kwa Mdude Mpaluka Nyagali.
Kusudi.
Kwamba mnamo tarehe 18 Septemba 2024 siku ya Jumatano muda wa saa 05:57 jioni, nilipata taarifa kutoka kwa msamaria mwema kuhusu uhai wangu. Msamaria huyo alinijulisha kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza nitekwe na kupotezwa kabisa katika dunia. Nimeshindwa kupuuza taarifa hizi kwasababu ya matukio mengi ya watu kutekwa na kupotezwa akiwemo mjumbe wa sekretarieti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA ambaye alitekwa na watu wenye silaha na pingu akiwa ndani ya basi la abiria kisha baadaye mwili wake ukaokotwa Ununio Dar es Salaam ukiwa umeharibiwa na kumwagiwa tindikali. Lakini pia nimesita kupuuza taarifa hizo kutokana na uhusiano wangu na utawala wa Rais Samia hasa pale serikali yake iliponikamata na kunishikilia kinyume na sheria kwa siku saba mimi na wenzangu kwa tuhuma za uongo za uhaini mwezi August 2023.
Hivyo basi kupitia barua hii nawajulisha ndugu, jamaa, marafiki, watanzania na jumuiya za kimataifa kwamba; lolote baya litakalonipata Rais Samia Suluhu Hassan ndiye atakuwa mtuhumiwa wa kwanza na atawajibika yeye kizazi na kizazi mpaka siku Yesu Kristo atakaporudi.
0 Comment
Leave a Comment