News Details

Bandari, Michezo, Elimu, Kila Sekta - Madudu Au Utani Wa CCM

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Kutokana na maoni ya watanzania, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imefeli katika kila nyanja kwani wananchi wanasema hawaoni sehemu ambayo serikali imefanikiwa katika kutatua changamoto zao. Huduma za jamii kama maji, umeme, afya na elimu  na miundombinu bado ni tatizo kubwa. Serikali ilisaini mkataba wa bandari licha ya wananchi kuupinga kwa kuwa wa unyonyaji. Leo hii wafanyakazi wa bandari wanaambiwa wachague kati ya kubaki Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) au kuandika barua ya kuacha kazi na moja kwa moja kuajiriwa na DP World jambo ambalo limetiwa mashaka na wananchi kuwa ni njia ya kupunguza wafanyakazi kwa kuwa kama DP World kweli wana nia ya kuwaajiri walitakiwa watoe mikataba hiyo kwa wafanyakazi ili wafanyakazi wa bandari wafanye maamuzi sahihi. 

Sekta ya elimu imeonyesha kufa nchini kwani tuna wenye vyeti wengi kuliko walioelimika na hivi karibuni serikali imekuja na taasusi mpya kwa ajili ya elimu ya juu ya sekondari lakini taasusi hizo hazijaonekana kulenga kuboresha sekta ya elimu. Katika karne ambayo taifa letu linatakiwa kupiga hatua kiuchumi ujasiriamali ulipaswa kuwa somo katika mtaala wetu wa elimu lakini sii hivyo na taasusi za biashara hazifundishi ujasiriamali. Nchi yetu inategemea kilimo kama mgongo wa uchumi lakini taasusi zenye somo la kilimo ni moja tuu. Pamoja na hayo bado miundombinu ya shule zetu zina changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa madawati, vyoo na vifaa vya kufundishia. Kwa upande wa michezo, ni kwa miaka mingi sasa wizara ya michezo imekuwa wizara ambayo inapelekewa viongozi ambao wameharibu kwenye sekta nyingine. Kwa kuangalia tija na ajira inayopatikana katika sekta ya sanaa na michezo, serikali ilipaswa kuichukulia kwa umakini sekta hii kwa kuweka viongozi walio na maono. 

 

Mageuzi pekee katika nchi yetu yataletwa na #KatibaMpya lakini hatuwezi kupata #KatibaMpya kwa kuongea tuu mtandaoni bali kwa vitendo pia kila inapohitajika. Kama wananchi inabidi tushiriki maandamano na harakati nyingine kuhakikisha tunaikomboa nchi yetu. Lazima wananchi hasa vijana tuachane na ujinga, uchawa na upumbavu na tuwe tayari kuipigania nchi, . tuwe wa kweli na makini katika kuleta mabadiliko. Tushirikaiane kupata #KatibaMpya .

#ChangeTanzania   #WenyeNchiWananchi 



ENGLISH VERSION

According to the opinions of Tanzanians, the government under the ruling party has failed in every aspect as citizens do not see the areas in which the government has succeeded in solving their challenges. Social services such as water, electricity, health, education and infrastructure are still a big problem. The government signed the port agreement with DP World despite citizens opposing it for being exploitative. Today, Tanzania port workers are being told to choose between remaining with their jobs at the Tanzania Ports Authority (TPA) or writing a letter of resignation and directly being employed by DP World. The move has been translated as a hidden agenda by the government to reduce its workers as there has not been any formal statement regarding the matter by DP World as if it truly intends to hire these workers it would have only been smart to hand over them their contracts beforehand so the workers can make an informed decision.  

 

The education sector has shown to be dying in the country as we have more certificate holders than those who are truly liberated by education. Recently the government has come up with new high school combinations but these combinations are seen to improve the education sector for the better but the worse. In a century where our nation needs to make strides in economic progress, entrepreneurship should be a subject in our education curriculum, but that is not so and business related combinations do not teach entrepreneurship in their courses. Our country heavily depends on agriculture as the backbone of the economy, but there is only one combination that has agriculture as a subject. Despite this, the infrastructure of our schools still has many challenges, including the lack of desks, sanitation facilities and teaching materials. The arts and sports sector also falls behind as for many years now the ministry of sports has been a ministry that is led by leaders who are seen to fail in other sectors. Looking at the productivity and jobs created by the arts and sports sector, the government is supposed to take this sector seriously by appointing visionary leaders.

 

The only reform in our country will be brought by a new constitution but we cannot get a new constitution just by talking online but also in action whenever needed. As citizens, we have to participate in protests and other movements to ensure that we liberate our country. Citizens, especially young people, must give up ignorance, and stupidity and be ready to fight for the country by working together to attain a new constitution.

#ChangeTanzania   #WenyeNchiWananchi

0 Comment

Leave a Comment