News Details

Umuhimu Wa Maoni Ya Wananchi Kwenye Katiba

Kwa kuwa #WenyeNchiWananchi, katiba inatakiwa kwa asilimia 100 kotokana na wanachi na mamlaka yote kubaki kwa wananchi. Mwaka 2012 Rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete aliunda Tume ya mabadiliko ya katiba chini ya Jaji Mstaafu Joseph Wariba. Tume hiyo kwa kutambua umuhimu wa maoni ya wananchi ilihakikisha inapata maoni ya wananchi Tanzania nzima. Tume ilifanya mikutano 1942 katika maeneo mbalimbali ya nchi hii kwa kutumia njia shirikishi ambayo iliwasaidia kuja na Rasimu ya #KatibaMpya bora ambayo kimsingi ndio Watanzania wanaitaka. Lakini Rasimu hii ilikwamishwa na Bunge la katiba ambalo kwa asilimia kubwa lilikuwa na wawakilishi kutoka serikalini ambao waliona kuwa mamlaka na maslahi yao yote ambayo wananchi wameona kuwa wanayatumia vibaya yamedhibitiwa sawasawa. 

 

Rais aliyefuata wa awamu ya tano alisema yeye #KatibaMpya sio kipaumbele chake na kusema kuwa yeye kipaumbele chake ni kujenga nchi kwanza bila kuthanini gharama kubwa ya pesa za Watanzania zilizotumika katika mchakato huo. Nchi hujengwa kwa utawala bora ambao unatokana na katiba bora yenye maoni ya wananchi. Na katika awamu hii udhaifu wa katiba hii ulionekana zaidi kwa kuwa na kiongozi anayefanya maamuzi kwa matakwa yake na kuvunja katiba wazi bila kuwajibishwa wala kuhojiwa na yoyote.

 

Jirani zetu Kenya wanafaa kuwa mfano bora kwetu katika upatakinaji wa katiba yao iliyopatikana August 2010. Ambapo baada ya machafuko yaliyotokea 2007-08, waliunda tume ya watu 9 ambapo ilikuja na Rasimu mbili za katiba ambazo zilileta mvutano mkali wa kimawazo lakini mwisho wa siku walipata katiba bora yenye maoni ya wananchi. Kenya imepiga hatua katika masuala ya mengi ya kikatiba ikiwepo uhuru wa mahakama, tulishuhudia Kesi iliyofunguliwa na Raila Odinga akipinga matokeo ya Urais ya William Ruto mwaka 2022, kitu ambacho Tanzania kwenye katiba yetu hakipo na hakijawahi kutokea. Jaji David Malaga mnamo septemba 19, 2017 alifuta uchaguzi Kenya na kuamuru urudiwe. Hii ndio faida wanayopata Kenya kwa kuwa na katiba ambayo ni matokeo ya ushiriki wa wananchi

 

Maoni ya wananchi katika kuunda #KatibaMpya yanatakiwa kuzingatia makundi yote ya wananchi na makundi maalum katika kutoa ushiriki ili kusiwepo na viashiria vyovyote vya ubaguzi.  Wananchi ndio wanaotakia mema nchi yao hii inathibitika katika Rasimu ya Jaji Warioba, ambapo wananchi walitoa maoni mazuri kama kuwa na serikali tatu, maoni yanayoendana na demokrasia ya vyama vingi, uwepo wa tume ya maadili katika katiba, kuweka muswada wa haki za binadamu, kupunguza mamlaka ya Rais, tume huru ya uchaguzi, wagombea binafsi, kupinga matokeo ya uchaguzi, uhuru wa mihimili yetu kama Serikali (utendaji), Bunge na Mahakama na mengineyo mengi ambayo wananchi walipenda yawepo katika katiba ya Tanzania.Tanzania mpya itastawishwa na katiba bora, katiba ambayo wananchi watakuwa wasemaji wa mwisho ambayo mamlaka  yatarudi kwa wananchi  na yatalindwa kikamilifu. 

 

 #KatibaMpya #ChangeTanzania.

6 Comment

  • XABMKgSIjPE
    April 29, 2024

    KNzXqCRSMxLcODFh

  • XABMKgSIjPE
    April 29, 2024

    KNzXqCRSMxLcODFh

  • XABMKgSIjPE
    April 29, 2024

    KNzXqCRSMxLcODFh

  • dWkgUKhNBpQyt
    May 3, 2024

    tDoTMYvCNclL

  • dWkgUKhNBpQyt
    May 3, 2024

    tDoTMYvCNclL

  • dWkgUKhNBpQyt
    May 3, 2024

    tDoTMYvCNclL

Leave a Comment