News Details

Kwa Nini Uchawa Na Upotoshaji Vyakithiri Nchini?

Hivi karibuni kuna mwana CCM ameibuka na kusema kusifia Rais Samia kwa kila kitu ni maagizo ya chama, na hivyo kila mtu anawajibu kumsifia kwa kila jambo. Hii hali imezua suala linalojulikana kama uchawa, kuna madhara makubwa sana kutoka na hali hii ya uchawa sababu, uchawa umekuwa ni kusifia kila kitu bila kuangalia changamoto zinazowakabili wananchi, kwa maana nyingine uchawa ni kuficha changamoto zote na kuzifukia ili zisitatuliwe matokeo yake inaleta changamoto kubwa sana kwa wananchi.


Suala la upotoshaji wa taarifa muhimu za serikali limekuwa sugu nchini,  viongozi na baadhi ya wananchi wamekuwa wakijikita katika kusifia utendaji wa Rais kuliko majukumu yao hasa ambayo Watanzania wamewaweka madarakani ili wayatimize. Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Samia imekuwa na miradi na utekelezaji mambo kadha wa kadha kama uwekezaji, ujenzi wa miundombinu mbalimbali kama barabara, reli nk. Ujenzi wa vituo vya afya nk. Yote hayo yakiwa yanafanyika kwa fedha za wananchi au mikopo ambayo pia hulipwa kwa fedha za wananchi. 

 

Uchawa ni kielelezo tosha cha serikali kukosa uwajibikaji katika Taifa hili kiasi cha kutafuta nguvu ya ziada ili kupamba miradi mibovu au mikataba ambayo haina maslahi na nchi hii, Waswahili walisema kizuri chajiuza kibaya chajitembeza. Kama serikali ingekuwa na uwajibikaji mzuri na kusikiliza maoni ya wananchi kwa usahihi isingekuwa na haja ya kuweka machawa kuhamasisha wananchi kukubaliana na kile wanachofanya kwa kuwa miradi na mikataba ingeonekana namna inavyonufaisha wananchi. 

 

Chanzo cha tatizo la uchawa na upotoshaji kwa umma lilianza pale ambapo watu waliotumia #UhuruWaKujieleza kukosoa serikali kupata matatizo kama kupokea vitisho, kutekwa, kupotezwa, kupigwa risasi, na hata kuuawa bila watu wanaofanya matukio hayo kujulikana na kuchukuliwa hatua. Hivyo watu katika kulinda vibarua vyao na kukosa uzalendo wakatumbukia kwenye wimbi la uchawa na upotoshaji kwa umma bila kujua kuwa wanakuza tatizo zaidi ya kulimaliza kwa kukabiliana nalo na kuzidi kuiambia serikali ukweli pale ambapo wanakosea.

 

Ni wazi kuna mambo mengi yanaenda mrama katika nchi yanayosabaishwa na serikali yetu, kama utekaji wa wananchi hasa wafanyabiashara, kunyanyasa Maasai katika ardhi yao, kuporwa ardhi na mifugo, mikataba mibovu, miundombinu iliyo chini ya viwango, uongo wa serikali kwa wananchi, na mengine mengi ambayo hata serikali huficha na kutenda bila idhini ya wananchi kama ilivyokuwa katika mkataba wa bandari, kwa kuwa mkataba huo ulivuja bahati mbaya. Pamoja na hayo ilitumika nguvu kubwa ya uchawa kuutetea mkataba huo kwa upotoshaji mkubwa na mkataba huo ulipitishwa.

 

Je nini kifanyike kukomesha uchawa na upotoshaji ? 

 

Ukweli ni kwama mamba haya yanahitaji zaidi sauti ya wananchi ipazwe kwa nguvu zote ili kuinusuru nchi yetu kutoka katika serikali isiyojali na kuheshimu wananchi. Ifahamike kuwa yote hayo yananfanyika kwa kuwa serikali ina mamlaka ya kuendesha kila kitu katika nchi hii na si wananchi. Wana uwezo wa kuvunja ibara ya 8 ambayo inatoa mamlaka kwa wananchi kwa kuwa ina uwezo wa kijilimbikia madaraka yote kwa kuwa katiba inawalinda na wananchi hawezi kuwafanya chochote.

 

Ili Tanzania kuonekana ina wananchi wanaotambua wajibu wao na kuwajibika ni uzalendo wa kuonyesha uwezo wao katika kudhibiti madaraka ya serikali na kuyarudisha kwao. Hili litawezekana kama wananchi wataamua kutafuta #KatibaMpya ambayo ndio chanzo cha udhaifu wote ambao wananchi wako nao sasa. #KatibaMpya ambayo imeandikwa na wananchi lazima itasimamia vizuri masuala ya uchaguzi wa viongozi na namna ya kuwawajibisha kwa kuwa hapa ndipo linapozaliwa tatizo la viongozi ambao wanazalisha uchawa na upotoshaji kwa umma. Na kusababisha wananchi kufumbia macho maovu yao. #KatibaMpya , katiba bora lazima ipatikane kwa maslahi ya wananchi. 

 

#KatibaMpya #WenyeNchiWananchi  #ChangeTanzania

2 Comment

  • GuaESRVtg
    April 20, 2024

    mxJItPZgbah

  • GuaESRVtg
    April 20, 2024

    mxJItPZgbah

Leave a Comment