News Details

Vijana Wanamageuzi Wako Wapi? Tunaondokanaje Na Uchawa Wa Vijana?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya  #ChangeTanzania 

Uchawa umeshika kasi katika taifa kiasi cha kuchukulia kama kazi nyingine. Hii ni aibu kwa taifa, kwani machawa husifia mambo ambayo hawatakiwi kusifia wakijua fika athari zake katika jamii.  Hawa ni watu hasa vijana wanaounga mkono chochote kile kinachofanywa na serikali hata kama kinaumiza jamii. Ni vijana waliogeuka kuwa wapambe wasiojali maslahi ya Taifa kwa ujumla, wanaotumikishwa na wanasiasa kuwapigia debe kwa malengo ya kisiasa na sio Taifa.

 

Machawa wamekuwa wakitumika kuhamasisha mikataba mibovu nchini ili hali serikali ikizidi kupuuza maoni ya wananchi wengine. Hali ya kuaminisha vijana kuwa ili uwe salama ni lazima uwe katika mfumo wa chama tawala ni moja kati ya mambo yanayochangia uwepo wa machawa. Pamoja na hilo, mfumo wetu wa elimu hauzalishi watu wanaoweza kujitegemea hivyo vijana kutaka kutafuta njia rahisi ya kutengeneza kipato kwa njia ya uchawa.  

 

Uchawa ni hatari kwa taifa kwani kizazi chetu kitaumia, rasilimali zetu zitaenbdelea kuibiwa, na maendeleo hayatakuwepo. Inabidi tuboreshe mfumo wetu wa elimu ili tupate elimu yenye kujibu matatizo ya jamii, na kuuwa uchawa. Elimu bora itajibu swala la umasikini na tukiondoa umasikini, uchawa utakufa. Vijana wana nguvu kazi kubwa lakini tatizo linakuja kwa kila kijana kuweza kujitathmini ili kujua nafasi yake katika kuleta mageuzi na maendeleo kwenye taifa. Vijana lazima tuelewe kuwa tuna jukumu kubwa katika taifa hili kwa kututumia uelewa wetu na kuachana na propaganda za kijinga na kuweza kusimamia ukweli. Vijana tunaojitambua tusichoke kupiga kelele, tusichoke kuelimisha vijana wengine juu ya hitaji la #KatibaMpya kama suluhu ya matatizo yetu. 

#ChangeTanzania  #WenyeNchiWananchi  #MariaSpaces 



ENGLISH VERSION

Uchawa has gained momentum in the nation to the point that it is considered as any other job. This is a shame for the nation, because machawa praise things that they should not praise, knowing their effects in society. These are people, especially young people, who support whatever the government does, even if it hurts the community. They are young people who have turned into buffoons who do not care about the interests of the Nation as a whole, who are used by politicians to promote their political goals and not for the Nation.

Machawa have been used to promote bad contracts in the country so that the government increasingly ignores the opinions of its citizens. The ongoing belief that convinces young people that in order to be safe one must be in the ruling party system is one of the factors that has contributed to the existence of Machawa. Despite that, our education system does not produce people who can be self-reliant, hence young people seek easy ways to make an income.

 

Uchawa is dangerous for the nation as it creates an environment that favors our resources to continue being exploited for the gains of those in power, thus development will not be achieved. We have to improve our education system so that we can get an education that responds to the problems of society. Better education will answer the question of poverty and if we eliminate poverty, thus putting an end to uchawa. Young people are a great workforce but the problem comes for every young person to be able to evaluate themselves to know their role in bringing about reform and development to the nation.

 

Young people must understand that they have a big responsibility towards the nation by using their understanding and abandoning stupid propaganda and being able to stand for the truth. Self-awared young people should not get tired of raising their voices and educating other young people about the need for a new constitution as a solution to our problems.

#ChangeTanzania   #WenyeNchiWananchi  #MariaSpaces

0 Comment

Leave a Comment