News Details

Gharama Za Maisha Kupanda, Je CCM Nchi Imewashinda?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Wananchi wanahitaji huduma za kijamii na bidhaa mbalimbali za kuwezesha maisha yao ya kila siku lakini gharama zimekuwa zikipanda kadri siku zinavyoenda. Bidhaa kama sukari ambayo ilikua shilingi 1,500/=  kwa kilo kwa sasa ni shilingi 5,000/=. Kama tungetumia vizuri ardhi yetu, tungeweza kuzalisha miwa ili tupate sukari, mpunga kwa ajili ya mchele nk. Lakini tunalalalmika kila mwaka kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa za vyakula kwa sababu serikali imeshindwa kuweka mipango madhibuti ya kuwezesha uzalishaji wa ndani. Nauli zimepanda mara mbili ndani ya mwaka mmoja, 

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imekuwa kama chombo cha kutangaza bei mpya badala ya kuwa mdhibiti kwani serikali inajua wananchi wanapitia maisha magumu. Pamoja na upatikanaji wa huduma ya kuendelea kuwa changamoto kubwa sana zinazopelekea kero kwa wazalishaji na wafanyabiashara wanaotumia umeme kushindwa kutekeleza shughuli zao za kiuchumi na hivyo kudorora kwa biashara zinazo tegemea nishati hiyo, gharama ya uniti za umeme zimepanda kiasi kwamba aliyekuwa akitumia umeme wa shilingi elfu kumi kwa mwezi hawezi tena kufika na uniti hizo hizo za umeme kwa sasa.  Akili za viongozi wetu si za kutatua matatizo ya wananchi bali wanajadili kupeleka huduma ili wapate kura, wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi na si ya wananchi. Wananchi waendelee kuunga mkono maandamano ya CHADEMA kuteteta maslahi ya wananchi. 

#ChangeTanzania  #WenyeNchiWananchi  #MariaSpaces 



ENGLISH VERSION

Citizens need various social services and products to facilitate their daily lives but the costs have been increasing as days go by. Food products like sugar which used to be 1,500 shillings per kilo is now 5,000 shillings. If we used our land well, we could cultivate sugarcane for sugar production, and paddy for rice enough to meet the domestic supply but instead we sit down and complain every year about the rise in the prices of food products because the government has failed to put in place strong plans to facilitate local production. Bus fares have gone up twice within one year, and the Land Transport Regulatory Authority (LATRA) has been just a tool used by the government to announce new prices instead of regulating the prices. Access to electricity service continues to be a challenge causing even more problems for producers and traders who depend on electricity to carry out their economic activities, the cost of electricity units has risen to such an extent that an individual who could survive on a ten thousand worth units can no longer survive a month with the same. The minds of our leaders are not directed towards solving the problems of the people, but they are focussed on delivering services to get votes, they are there for their own interests and not for the people. Citizens should thus continue to support the CHADEMA protest to defend the interests of the citizens.

#ChangeTanzania   #WenyeNchiWananchi  #MariaSpaces

0 Comment

Leave a Comment