News Details

CCM Kutumia Dola Kushika Dola Tunaondokana Vipi Na Usultani Wao?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Chama Cha Mapinduzi kimekua kikiongoza Tanzania tangu taifa letu lipate uhuru na kimeendelea kubaki madarakani kwa zaidi ya miaka sitini sasa. Kuendelea kubaki madarakani kwa CCM si kwa ridhaa ya wananchi bali dola kwani CCM imeamua kujichukulia madaraka kupitia dola na kujihakikishia kuwa inabaki madarakani kwa kutumia nguvu na mabavu. Jambo hili limepelekea unyanyasaji, ukandamizaji na kupotea kwa haki za bindamu kwa wananchi. Tumeshuhudia watu wakibambikiziwa kesi za uongo, waandishi wa habari wakikamatwa na kuwekwa ndani kwa kuikosoa serikali, vyama vya upinzani vikinyimwa uhuru wa kutekeleza majukumu yao kikatiba na serikali kupuuzia matakwa na maoni ya wananchi ambao ndio wenye mamlaka ya kweli kwa kuweka mbele maslahi ya chama.  

 

Katiba yetu ambayo ni sheria mama haijatenganisha kati ya chama tawala na dola kwa kumpa Rais mamlaka makubwa kupelekea uongozi wa kiusultani, kwani vyombo vyote vya uendeshaji wa nchi yeye ndiye anachagua viongozi wake. Hakuna mipaka ya kuheshimiana kati ya mihimili ya serikali, na hili si jambo zuri kwa maslahi mapana ya taifa. Hii imeonekana kwenye masuala kama ya wamasai wa Loliondo na Ngorongoro kutolewa kwamabavu kwenye makazi yao na serikali  kuwanyimwa huduma za msingi kama njia ya kuwalazimisha kuhama kwenye makazi yao. Katika swala hili, bunge limefumbia macho na mahakama pamoja na kusuluhisha baadhi ya kesi zilizofunguliwa kwa manufaa ya wananchi bado haijachukua hatua yeyote pale serikali ilipokiuka maamuzi ya mahakama. 

 

Katika mfumo huu hakuna mtu yeyote wa serikali anayeweza kuhoji chama na kumpiga kiongozi wa chama lakini kiongozi wa chama ana uwezo wa kumuwajibisha mtendaji wa serikali. Ili kurudisha mamlaka kutoka kwenye dola na kurudi kwa wananchi ni lazima tupate katiba bora na watu wenye nia ya dhati ya kusimamia katiba ili tuondokane na chama dola bali  chama kinachotambua kuwa kinawajibika kwa wananchi. 

#ChangeTanzania  #WenyeNchiWananchi  #MariaSpaces 



ENGLISH VERSION

Chama Cha Mapinduzi has been leading Tanzania since independence and has continued to remain in power for more than sixty years now. CCM continuing to remain in power has not been with the consent of the people but because CCM has decided to take power through the government and assure itself that it remains in power by using force. This has led to abuse, oppression and the loss of human rights for citizens. We have witnessed people being accused of false cases, journalists being arrested and imprisoned for criticizing the government, opposition parties being denied the freedom to carry out their constitutional duties and the government ignoring the wishes and opinions of the people who have the real power by putting the party's interests first.

 

Our constitution, which is the mother law, has not clearly separated between the ruling party and the state by giving the President too much powers of authority leading to the sultanate leadership, since the president elects all the leaders of the governing bodies of the country. There is no accountability relations between the branches of government, and this is not good for the wider national interest. This has been seen in issues such as the Maasai people of Loliondo and Ngorongoro being forcibly removed from their homes and the government denying them basic services as a way of forcing them to move. In this matter, the parliament has turned a blind eye and the court on the other hand, while it resolved some cases opened by the citizens in favor of the citizens it has not yet taken any action when the government is seen to have violated the court's decisions.

In this system, no one in the government can question the ruling party CCM, but the party leader has the ability to hold the government executive accountable. In order to return power from the government to the people, we must get a better constitution that will put in place enable us to get a ruling party that recognizes that it is responsible to the people.

#ChangeTanzania   #WenyeNchiWananchi  #MariaSpaces

0 Comment

Leave a Comment