News Details

Maandamano Ndo Lugha Wanayoielewa CCM - Tumejipangaje?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Mafanikio ya nchi yanapangwa na uongozi uliopo madarakani. Hali mbaya ya nchi yetu inasababishwa na viongozi wetu kutofikiri vizuri na kukosa maoni ya mbele, matokeo yake imepelekea nchi kuingia kwenye matatizo mengi. Uchumi wetu sio imara, nchi inakosa nishati ya muhimu ya umeme inayopelekea uzalishaji mdogo na serikali imekosa jawabu. Ongezeko la bei imepelekea maisha kuwa magumu kiasi cha wananchi kukosa milo mitatu kwa siku. Vyombo vya dola vinashindwa kufanya kazi katika misingi ya katiba na kutambua mipaka yake. Bunge halina nguvu yeyote kwani limekua sehemu ya serikali na si tena sehemu ya wananchi. Wananchi hawana sehemu ya kuwasilisha maoni na matakwa yao kwa serikali na wanaojitahidi kufanya hivyo wametishiwa vikali. Vyombo vya habari vinazuiwa kuripoti baadhi ya taarifa kwa umma. Katika nchi ya kidemokrasia, uhuru wa wananchi kutoa maoni yao juu ya mambo yanayowasumbua na juu ya miendendo ya serikali ni jambo la msingi. Serikali kushindwa kusikiliza hoja za wananchi imepelekea maandamano kuwa njia pekee ya kuifanya isikilize kero hizo. 

Pamoja na maandamano kuwa ni haki ya kikatiba bado serikali kwa kupitia jeshi la polisi limekua likiingilia na kuvuruga maandamano kinyume na sheria. Wananchi wameisihi serikali iache kutumia nguvu za jeshi la polisi kuzima hoja badala ya kusikiliza hoja na iache jeshi la polisi lifanye kazi yake ya kulinda raia. Wananchi wamehimizana kushiriki kikamilifu kwenye harakati za maandamano ili kuishinikiza serikali kuchukua hatua zinazohitajika kuleta mabadiliko nchini. 

#ChangeTanzania  #WenyeNchiWananchi  #MariaSpaces 



ENGLISH VERSION

The success of the country is planned by the leadership in power. The bad situation of our country is caused by our leaders lacking vision to think forward and as a result has led the country into many problems. Our economy is not stable, the country lacks important services such as power which is crucial for economic production. The increase in prices has made life difficult for the people such that some still fail to have three meals a day. State institutions fail to operate on the basis of the constitution and recognize its limits. The parliament has lost its power in being the voice of the people as it has become part of the government. Citizens do not have a place to present their views and opinions to the government and those who strive to do so are severely threatened. The media is restricted from reporting some information to the public, something that goes against the principles of a democratic country as in a democratic country, the freedom of citizens to express their opinions on things that matter as well as on the actions of the government is of fundamental importance. The government's failure to listen to the people's arguments and opinions has left protests as the only way to make it listen to those concerns.

 

Despite protest being a constitutional right, the government through the police force has been interfering and disrupting protests against the law. Citizens have pleaded with the government to stop using the power of the police force to shut down their opinions instead of listening to their opinions and let the police force do its job of protecting the citizens. Citizens have encouraged each other to actively participate in the protest movement to pressure the government to take the necessary steps to bring about change in the country.

 

#ChangeTanzania   #WenyeNchiWananchi  #MariaSpaces

0 Comment

Leave a Comment