News Details

Yuko Wapi Dr Mpango? Where Is Dr Mpango?

Hili swali sasa limefika hatua mbaya kidogo, serikali imekuwa na utamaduni wa kudanganya kuhusu wapi walipo viongozi au safari wanazofanya viongozi, Kwa mwezi sasa Dr Mpango haonekani, lakini pia amewakilishwa kwenye shughuli alizotakiwa kufanya kama Makamu wa Rais, Dr Mpango haonekani popote na wasiwasi umeanza kuwa mkubwa, kuna mengi yanasemwa mfano Yuko kwenye Matitabu Korea Kusini na wengine wanasema yuko Israel kwa matibabu, Lakini hayo yote sio muhimu, kwa nini Dr Mpango asijitokeze kutuliza hali hii ambayo imejenga wasiwasi wenye haki miongoni mwa wananchi ?

Juzi ameibuka  Waziri Mkuu na kusema Dr Mpango yuko nje ya nchi kwa majukumu bila kusema ni majukumu gani na wapi imeleta shida kubwa kuliko ya awali. Waziri Mkuu anadanganya umma, Kwa sababu kama Mpango yuko nje ya nchi, yuko wapi na anafanya nini? Toka lini Taarifa kama hii ikawa ni siri kwa umma? Toka lini makamu wa Rais akaenda nje ya nchi kwa mwezi mzima na kusiwe na Taarifa yoyote maalum kwa umma?

Kwa uchunguzi uliofanyika (kupitia wadau mbalimbali ) ,kuanzia uwanja wa ndege na kwa  wananchi na wafanyakazi wanaofanya shughuli zao uwanja wa ndege, hakuna anayesema kaona makamu akisafiri, kama Dr Mpango yuko nje ya nchi hakutoka kwa njia za kawaida. Hii inaashiria labda anaweza kuwa mgonjwa kwa kuwa hakuna uwanja wa ndege wenye kumbukumbu ya kumuona Mpango kwa mwezi sasa. Je alisafiri vipi kwenda nchi za nje na kusiwe na TAARIFA kwenye uwanja wa ndege wowote? Kwa nini Majaliwa hakusema Dr Mpango yuko nchi gani kwa shughuli gani ? Alichofanya Majaliwa ni kusema tu hayuko nchini ili kuondoa swali la kwanini ajaenda Katesh na Hanang kwenye maafa sababu yenye ni kiongozi namba mbili pale Rais anapokuwa nje ya nchi. Lakini hata ili la maafa ajaonekana wala kuzungumza chochote ? Yuko wapi Mpango?

Kama wananchi tunahoji Dr Mpango anafanya shughuli gani nje ya nchi mwezi mzima hakuna picha wala video moja, hakuna hata Taarifa tu kwenye media yoyote kuonyesha shughuli za Makamu wa Rais kwa mwezi mzima,  Hii inawezekana vipi?

Lakini pia hakuna shughuli yoyote ya kiserikali kwenye maeneo yaliyozoeleka, barabara anazotumia Dodoma na Dar hakuna msafara wake umeonekana, Kanisani hayupo , Dr  Mpango ni wa kuacha kusali mwezi mzima?  Kwa nini serikali inaficha jambo hili? Kauli ya Waziri Mkuu Dr Mpango kuwa nje ya nchi imeibuwa wasiwasi na Maswali mengi zaidi

Babati , Hanang na Kateshi huko Manyara kumetokea mtikisiko ambao umesababisha maafa na uharibifu wa miundo mbinu mbalimbali Hanang na Katesh, Inasadiliwa kwamba ni volkano inalipuka lakini serikali hapa pia inaonekana kuficha taarifa ili tope jepesi linalotembea ni nini? Ni kama Serikali imedanganya na kusema ni mafuriko ili kupoza na kuondoa wasiwasi kwa wananchi bila kujali kama tukili linaweza jirudia. Toka lini mvua ni matope laini vile? Je mvua ina uwezo wa kuporomosha mawe makubwa kutoka milimani na mlima kumwagika hayo ni mafuriko au kuna taarifa zilizojificha?

Hoja hii ya  Hanang na Katesh inaturudisha kwenye Hoja ya Mpango, kama Yuko nchini kwa nini asijitokeze kutembelea wahanga si mlisema yuko LIKIZO? anaendelea na LIKIZO? ili kuondoa hoja ya yuko LIKIZO ndipo Majaliwa ametumika kusema Mpango yuko nje ya nchi, Tunakuwa na waziri Mkuu asiye muwazi kwa nini? 

Hii inatukumbusha pia kipindi wananchi wanaulizia alipo Hayati Magufuli ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa yupo vizuri ana anaendelea na majukumu yake ya kawaida kuwa hatuwezi kukutana na Rais Kariakoo,  lakini matokeo yake kila mtu aliyashuhudia kuwa Rais alipatwa na umauti. 

Majaliwa anasema mitandao inasema uongo? inasema uongo gani? kwa Mpango ameonekana lini mara ya mwisho? Watu wanauliza alipo Mpango kwa sababu ni kiongozi ana dhamana ya ofisi wananchi wanatakiwa kujua viongozi wao wako wapi na wanafanya nini. Inakuwa  hivi ili kuwakinga viongozi. Kusema Mpango yuko Nje ya nchi haitoshi, lazima Mpango mwenyewe ajitokeze na kusema yuko wapi anafanya nini? Majaliwa ana sababu gani kufafanua alipo mtu HAI akiendelea na shughuli zake kama kawaida? kuna ugumu gani kwa serikali kuridhisha umma kwenye swali la msingi kabisa ya kwamba, Makamu wa Rais yuko wapi? ni swali linatakiwa kujibiwa na Mpango mwenyewe sio wasaidizi wake wala waziri Makuu. Ni Makamu wa Rais pekee ndiye anayetakiwa kuondoa wasiwasi huu ambao unaweza kuwa na nia njema au ovu haijalishi lakini cha msingi ni lazima wananchi wapate kujua alipo huyu kiongozi tena kwa kuona na kusikia kauli yake.

#ChangeTanzania

0 Comment

Leave a Comment