News Details

Madhara Ya Kufuta Umiliki Na Kuuza Kwa Mtu Mwingine Namba Za Simu Zinapokaa Miezi 3 Bila Kutumika.

Kuna utaratibu mbaya sana umewekwa namna ya usimamizi wa namba SIMU zinapokaa miezi mitatu bila kutumika, Utaratibu huu umelalamikiwa sana na pande zote. Yaani wale wanaopewa hizo laini bila kujua kwamba ilikuwa ni namba ya mtu hapo awali hivyo anaanza kupokea simu na message nyingi zisizo muhusu, hii ikiwa ni pamoja na kupigiwa simu kuitwa kwenye vikao na vikundi ambayo ahusiki navyo. Lakni kwa Upande mwingine mmiliki wa hiyo simu hapo mwanzo anapoteza kabisa mawasiliano yake ya namba hiyo kwa kuwa umiliki unaama na kuwa wa mtu mwingine,  lakini mara nyingi WhatssApp inabaki kwa mtu wa zamani na mmiliki mpya anaweza kutumia message za kawaida na kupiga simu pamoja na huduma za miamala. Mara nyingi kwa kuwa namba hii inakuwa imetumika kwenye mifumo mingi, mmiliki mpya hawezi kuitumia hiyo namba kwenye mambo mengi na kujikuta anasajili namba mpya.

Kwa watu wanaowasiliana na namba hiyo, mfano umetuma ujumbe wa kawaida unakwenda kwa mmiliki mpya, lakini ukitumia WhatsApp message inakwenda kwa mmiliki wa zamani. Hasara na hatari ya suala Hili masuala na taarifa nyingi za mmiliki wa zamani zinakwenda kwa mmiliki mpya, hivyo kama mmiliki mpya ni tapeli anakuwa amepata taarifa nyingi sana zikiwemo za kibenki na kadhalika. Hili suala linalalamikiwa sana, wengi wanasema namba inapofungwa asipewe mtu mpya bali iachwe mpaka itakapo sajiliwa tena na mmiliki yule yule, kwa sababu kuna watu wanafika hatua wanashindwa kumiliki simu ya mkononi hivyo kutotumia laini ya simu hiyo kwa muda, kuna watu wanasafiri nje ya nchi, wengine wanaugua na kuzima simu kwa muda, namba hizo zote zinafugwa na kuuzwa tena.

Sheria  hii inahitaji kuboreshwa ili kulinda usiri wa watumiaji wa simu na mifumo ya kidigitali. Changamoto ya laini isipotumiwa kwa miezi mitatu laini hiyo inatolewa au kuuzwa kwa mtu mwingine. Muda wa miezi mitatu ni mchache sana kwa kitendo kama hicho kufanywa na makampuni ya simu. Kuna sababu za msingi ambazo zinaweza kupelekea mtumiaji wa laini kutokuwa hewani kwa miezi mitatu kama vile Magonjwa , kusafiri kibiashara, kufilisika, kuwa maeneo yasiyo na mtandao husika , kukaa mahabusu, kuwa mashuleni kwa wanafunzi au kupitia changamoto ambazo unakuwa huna simu ya mkononi kwa wakati huo, hivyo si sahihi Laini ya simu kuuziwa mtu mwingine.

Kwa mfano  benki  usipotumia akaunti inafungwa lakini jalada linabaki kuwa lako, wanaweza kutoza kiasi chs fedha kurudisha hiyo akaunti baada ya kuandika barua au kuwataarifu kuwa unaomba akaunti yako irudishwe, lakini namba ya SIMU yenye mawasiliano na taarifa nyingi za mtu inaweza kuuzwa baada ya miezi mitatu. 

Ni hali ya kushangaza kwamba unawezaje kuuza namba ambayo tayari imetumika? Inafahamika mtu anaposajili laini ya simu anatumia kitambulisho cha taifa ambacho kina taarifa zake zote, pili kipindi cha matumizi ya laini hiyo watu hutunza mambo mbalimbali katika simu zao ambayo pengine ni ya siri kutoka kwa mwajiri wake, mchumba wake, mkewe au mumewe, Daktari wake nk. Ni jambo lisilowezekana kwa mtu laini yake inapouzwa au kufungiwa kueleza watu wote kwamba yeye si mtumiaji wa simu hiyo tena. 

Kufungwa kwa laini ndani ya miezi mitatu ni faida mojawapo waliyoipata matapeli wa mtandaoni kutapeli watu, watu hao wakijua wanatuma pesa kwa mtumiaji wa namba aliyepita ambaye wanamfahamu kumbe siye na namba hiyo kapewa mtu mwingine.

Sheria mbovu za mawasiliano  zimeleta mkanganyiko mbaya sana katika jamii, ili hali tuna Waziri anayeweza kushughulikia changamoto hii mara moja. Ingekuwa ni vyema namba zinazovunjwa kuwekwa kando na kama mtumiaji wa namba hiyo akitaka kuirudia namba yake iweze kufufuliwa na kuendelea na matumizi yake. Hii inasidia kulinda haki za mtumiaji ambazo zimeainishwa na sheria.  Hali hii inasababisha watu kusajili namba mpya kila mara na hii inauwa uimara, muendelezo  na utulivu wa mawasiliano. Hii ni hasara pia kwa makampuni ya simu kuzalisha laini kwa gharama kila wakati.

Sheria hii haijazingatia ustawi wa kiuchumi na jamii kwa undani, tunaamini mawasiliano imara ndio nguzo kubwa ya mambo mengi ya kiuchumi, mtu anapapota changamoto ya kutotumia laini ya simu kwa miezi mitatu ni wazi watu wake wote wa biashara walimtafuta kwa namba hiyo hivyo anahitaji kufanya mwendelezo wa alipoishia ili kuepuka kupoteza muda na kukosa watu wengine ambao kisingi wana mchango katika harakati za uchumi kwake.

Ni wakati wa kufanya mageuzi ya sheria mbovu hii ambayo haijazingatia vizuri haki za watumiaji wa laini za simu.

Tunatakiwa kuzingatia usiri wa Taarifa za Watanzania 

#ChangeTanzania

2 Comment

  • UfQzogDcyZhO
    July 2, 2024

    sbcUBOPy

  • UfQzogDcyZhO
    July 2, 2024

    sbcUBOPy

Leave a Comment