News Details

Nguvu Ya Umma Katika Kuleta Mabadiliko.

Nguvu ya umma ni namna ya wananchi wa kawaida hupigania haki zao, uhuru, na usawa kwa njia halali za kisheria bila kutumia njia za hatari. Hii ni haki iliyoainishwa na Katiba yetu ya Tanzania 1977. Wananchi wanapotumia nguvu ya umma wanakuwa na malengo ya kujenga Taifa lenye demokrasia, na kurudisha mamlaka kwa wananchi , Kuna mambo ambayo yanaweza tafsiriwa kama nguvu ya umma, kwa mfano  migomo, kususa, maandamano makubwa na hatua nyingine,  yakiwa na malengo ya mabadiliko makubwa ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Mara nyingi nguvu ya umma  ni mapambano au shinikizo la kudai haki kwa njia ya amani kwa nguvu ya raia,  wananchi huungana kwa sauti moja  kupambania kile wanachoamini ni haki yao na haitekelezwi na watawala, Kuna wakati Nguvu ya umma inaweza tumika kuondoa utawala ulipo madaraka kama wananchi wana hoja ya kuondokana nao, au wamechoshwa na uzembe, ukatili au kupuuzwa na watawala.

Tanzania historia ya watu kutumia nguvu ya umma kuleta mabadiliko uzoefu wa mara kwa marai sana kwa kuwa wananchi kila walipoamua kuandamana kudai haki au kupinga mambo yanayofanywa na serikali waliishia kukumbana na fujo za vyombo vya  dola na maandamano hayo kuzuiwa. Mwaka 2018 katia maandamano ya CHADEMA polisi  wakipiga risasi za moto na  kusababisha kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini. Mfano mwingine wa hivi karibuni ni maandamano ya kupinga mkataba wa bandari baina ya Tanzania na DP World yaliyondaliwa na kijana wa Bavicha Deusdedith Soka lakini licha ya maandamano hayo kufuata hatua zote za kisheria lakini walizuiwa na jeshi la polisi na waandamanaji  hao wengine kukamatwa na kupelekwa kituo cha polisi. 

Ni wazi katiba katika ibara ya 8 inatoa mamlaka kwa wananchi yaani #WenyeNchiWananchi, hivyo wana haki ya kuamua mambo muhimu yanayoendelea katika Taifa hili.ukweli kwa namna serikali yetu inavyoendesha mambo kwa sasa hatuwezi kuikomboa nchi hii bila nguvu kubwa ya umma, nchi nyingi zimefanikiwa kufika sehemu nzuri kwa wananchi kujitambua. Kuacha hofu na woga nyuma na kuchukua hatua, mfano Kenya mwaka 2007 katika kudai #KatibaMpya,  matumizi ya nguvu ya umma yalisaidia sana katika kutokomeza ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, Mwaka 2005, Walebanoni kwa kupitia maandamano makubwa ya amani walikataa majeshi ya Syria kuendelea kutawala nchi yao .

Hivi karibuni Tanzania imeingia mkataba wenye masharti magumu na hatari kwa rasilimali ya bandari zetu zote nchini. Serikali inaonyesha kuutetea mkataba huu japo ya watu mbalimbali wasomi kwa wasio wasomi kuukosoa mkataba huu kwa kuwa hauna maslahi kwa Taifa letu lakini serikali imeonyesha kutojali maoni ya wananchi ili kufuta mkataba huu baina ya Tanzania na DP World. Kwa kuwa katiba inatoa wajibu kwa wananchi kulinda maliasili na rasilimali, wananchi wameonyesha juhudi hadi za kwenda Mahakamani wakiwakilishwa na Wakili  Boniphace Mwabukisi  na wenzake kuupinga mkataba huu lakini mahakama nayo imeegemea upande wa serikali na kutofanikiwa. Vivyo hivyo hata kuhusu  #katibaMpya,  serikali imekuwa ikizunguka na kuchelewesha mchakato wa kupata #KatibaMpya ambayo itaweka mifumo ya nchi hii sawa na kuwa na mfumo wa utawala wa sheria yenye meno na kudhibiti kikamilifu ubadhirifu wa mali za umma.

  • Wananchi tumejipanga vipi katika kuhakikisha tunatetea maslahi  ya Taifa?
  • Je ni sawa kuendelea kukaa kimya huku rasilimali zetu zikiendelea kupotea?

Mahakama pekee iliyobaki kupinga mkataba wa bandari na kupata #KatibaMpya ni mahakama ya wananchi kutumia nguvu ya umma. Wachache wamekuwa wakijitoa kutetea maslahi ya umma lakini wananchi walio wengi wamekuwa wakishindwa kuunga mkono juhudi hizo kwa kuhofia madhara. Umoja wetu ndio utakaotuokoa kwa kuwa maandamano yenye kutumia nguvu ya umma yanaogopesha na hufanya watawala kutii nguvu ya umma inachotaka, kwa sababu hukusanya watu wengi pamoja kupinga uonevu na mateso yenye kuletwa na viongozi kwa kuleta dira mpya ya jamii yenye uhuru na haki zaidi na pengine kwa kutoendelea kuwaunga mkono wale walioidhinisha katiba yenye mifumo isiyofaa au ya zamani. Watu wengi wanapoamua kutounga mkono utawala mbaya, ufanyaji kazi wa mfumo unaanza kuwa mgumu sana. Pale watu wanapoamua kutotii mfumo ni lazima uanguke.. Hata kama serikali ikiamua kupinga  nguvu ya umma kwa sababu wana  silaha na fedha za kutosha, hawawezi  kukabiliana na maandamano yenye idadi ya kutosha kama wananchi wakisimama pamoja kudai haki kwa amani Kama kupinga mkataba wa bandari na kudai #KatibaMpya.  

#OkoaBandariZetu #KatibaMpya #ChangeTanzania

3 Comment

  • UJceSTglnXYz
    April 23, 2024

    JzZlbtpRc

  • UJceSTglnXYz
    April 23, 2024

    JzZlbtpRc

  • UJceSTglnXYz
    April 23, 2024

    JzZlbtpRc

Leave a Comment