News Details

Kukosekana Kwa Umeme Nchini.

Tatizo la uhaba wa umeme nchini linaathiri maisha ya watu na shughuli za kiuchumi, serikali ya  imekiri kupungua kwa kasi ya uzalishaji umeme hali inayopelekea kupatikana kwa umeme wa mgao katika maeneo tofauti ya nchi. Rais anasema kutokarabatiwa kwa mitambo ni sababu iliyosababisha kukosekana umeme, ametoa maelekezo kwa mkurugenzi mpya kwenda kupambana na changamoto na zimalizike kwa miezi 6 !! , Swali kubwa la kujiuliza ilikuwa mitambo ya umeme ikakosa ukarabati? Je kuna wanasiasa wowote walihusika? kuna wataalamu wamewajibika na hili tatizo la kutengeneza? Kwa nini wananchi wapata matatizo kwa matatizo ya kutengenezwa? au kutokana na uzembe wa watu?

Mapema Mei mwaka huu aliyekuwa Waziri wa Nishati, Januari Makamba, alisema Serikali  ipo katika mikakati kwa kipindi cha  miaka miwili kuhakikisha kuwa tatizo la upatikanaji wa umeme nchini linakuwa historia. Makamba aliyasema hayo kwenye maonyesho ya Wiki ya Nishati, alikiri kwamba  umeme bado ni changamoto na  bado haijawekwa sawa lakini kupitia mpango walio nao litamalizika na kuhusu uzalishaji wa umeme nchini, Makamba amesema umeongezeka kwa asilimia 11 kwa mwaka, ikilinganishwa na mwaka 2022 ambako kulikuwa ongezeko la asilimia 5.

Haikupita muda July 2023 Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la umeme nchini (TANESCO) ,Maharage Chande alisema katika kuongeza ufanisi uwajibikaji na utendaji wa kazi Shirika la Umeme nchini TANESCO, wamedhamiria kumaliza changamoto ya umeme ifikapo mwezi June 2024.  https://bit.ly/3ET9qHy Kauli hii inaonekana kuwa kama ghelesha kwa kuwa wanachopitia wananchi sasa hakisadifu maneno ya mkurugenzi huyo wa Tanesco kwa umeme umekuwa ukikatika kwa zamu katika maeneo yote ya nchi kwa muda mrefu hadi kufikia masaa 12. Hivyo Tanesco wanaposema wana mkakati wa kumaliza tatizo la umeme mpaka June 2024 ilitakiwa kuonekana juhudi za  kumaliza Tatizo kwa kuboresha huduma zaidi na si kurudi nyuma kwa hatua kadhaa.

Kukatika kwa umeme ni matokeo ya siasa ambazo zimesababisha maamuzi makubwa ya kitaalam yafanyike kisiasa, jinsi tatizo la umeme nchini Tanzania lilivyo kubwa na jinsi ambavyo ahadi zinazotolewa katika kila uchaguzi kuu na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) kuhusu tatizo la umeme kuwa historia zilivyokuwa na siasa au tatizo la umeme kutumika kukidhi malengo ya kisiasa.

Kwa miaka mingi sasa Tanzania imekuwa na tatizo sugu la siasa kuathiri mfumo wa umeme ambalo linaturudisha nyuma kila kukicha . Tangu wawekezaji binasfi waliporuhusiwa kuzalisha umeme mwanzoni mwa miaka ya 1990. Baadhi ya kampuni za wazalishaji binafsi wa umeme (Independent Power Producers) zilizoingia Tanzania zilikuwa ni IPTL, Richmond na Dowans. Wengi wa wazalishaji hawa huru walihusishwa na siasa za chama tawala, CCM. Lakini kuja kwao kuligubikwa na tuhuma za rushwa zilizosababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa mwanzoni mwa 2008. Hata hivyo Lowassa akizungumza Bungeni kabla ya kujiuzulu, alilalamika kuwa alionewa kwa kutuhumiwa na kuhukumiwa bila kusikilizwa, hivyo alijiuzulu ma maslahi ya chama chake na serikali.https://bbc.in/3ESoe9h

Tanzania imebarikiwa kila aina ya chanzo cha kuzalisha  umeme kwa maji, jotoardhi, na hata kwa upepo. Mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya upepo mkoani Singida haukuwahi kuanza. Pia nchi nzima ina fursa ya kuzalisha umeme kwa jua, uwezo wa kuzalisha umeme kwa gesi pia upo wa hali ya juu  kwa zaidi ya futi za ujazo trilioni 60. Upatikanaji wa madini ya urani nao pia unaipa Tanzania nafasi ya kuzalisha umeme wa nyuklia kama serikali ikitaka. Tafiti zilizothibitishwa zinaonesha kuwa kuna madini ya urani katika mikoa ya Ruvuma, Dodoma, Singida, Manyara na Arusha japo hayajaanza kuchumbwa. Kwa kifupi Tanzania haitakiwi kuwa na matatizo ya umeme. Inatakiwa iuze umeme nchi za nje. Lakini rasilimali kama hizi huwa haziwezi kuifaidisha nchi kama siasa zake hazikidhi mahitaji na kuleta tija kwa manufaa ya watu wake. 

Hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa September 20, 2023 amefungua Kongamano la Tano na Maonesho ya Nishati Tanzania na amesema kwamba Serikali imedhamiria kuwa Mzalishaji mkubwa wa nishati na kuwa na umeme wa kutosha utakaopatikana kwa urahisi na nafuu na ziada itauzwa nje ya Nchi. amesema serikali inaendelea na utafutaji wa gesi, tunataka tuwe Wazalishaji wakubwa wa nishati, tuwe na umeme wa kutosha utakaopatikana kwa urahisi na nafuu na ziada tutauza nje ya Nchi.

Kwa kauli kama hizo inaonyesha kuwa serikali imekuwa ikifanya mambo tofauti na kuongea tofauti. Hali ya umeme imezidi kuwa tete nchini na kusababisha hasara kwa wananchi na hasa sekta ya kiuchumi, lakini Waziri Mkuu anasema kuwa tutuaza umeme nje. Nchi hii imekuwa na miradi mingi ambayo inaendelea nchini ambayo inahitaji na itahitaji umeme wa kutosha ili kuleta ufanisi katika utendaji wake. Mfano treni ya umeme na mingineyo.

  • Kwa hali hii ya kusuasua kwa umeme je tutafanikiwa kuibadili Tanzania na kuwa moja kati ya nchi zilizoendelea? 
  • Kila mara zimekuwa ni sababu za kimazingira ambazo zinazochangia uzalishaji wa umeme kushuka, Je serikali yetu imekosa kabisa ubunifu wa namna ya kupata umeme licha ya kuwa na vyanzo tofauti tofauti vya kuzalisha umeme?

Ingekuwa ni vyema Serikali ikawajibika kwa maslahi mapana ya wananchi kwa kuzingatia wakati uliopo na vizazi vijavyo. Nishati ni chanzo muhimu cha kuleta msisimko wa uchumi.  Nchi yetu imebarikiwa vyanzo vingi vya kuzalisha umeme lakini ifike mahali vinufaishe Watanzania na hata mataifa jirani. Ili kufanikisha hayo tunatakiwa kupata katiba bora ambayo itakuwa na meno kwenye suala zima la uwajibikaji na wananchi kuwa na mamlaka, wasiporidhishwa na utendaji wa kiongozi huyo wawe na mamlaka ya kumtoa kwenye uongozi. Kwa kufanya hivyo tutapata uwajibikaji katika sekta zote na kuwa na Taifa bora. #KatibaMpya ni sasa.

#Change Tanzania

3 Comment

  • VMKbnhRXjuHzf
    April 23, 2024

    OKwrdzhWEi

  • VMKbnhRXjuHzf
    April 23, 2024

    OKwrdzhWEi

  • VMKbnhRXjuHzf
    April 23, 2024

    OKwrdzhWEi

Leave a Comment