News Details

Hotuba Ya Waziri Wa Fedha Na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba Madelu (Mb), Akiwasilisha Bungeni Mapendekezo Ya Serikali Kuhusu Makadirio Ya Mapato Na Matumizi Kwa Mwaka 2023/24.

Makadirio ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24 yameandaliwa kwa kuzingatia nyaraka na miongozo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikiwemo: Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 - 2025/26) ambao umezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020; Dira ya Maendeleo ya Afrika Mashariki 2050; Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063; Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030; Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2022 - 2027; makubaliano mengine ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

#ChangeTanzania

0 Comment

Leave a Comment