News Details

Tibaijuka : Uraia Pacha..Chanzo Chake, Tanzania Tunakosea Kuvua Watoto Wetu Uraia.

Anaandika Prof. Anna Tibaijuka, aliyekuwa Waziri

TIBAIJUKA : URAIA PACHA..CHANZO CHAKE :

Wakati tunapata uhuru wageni walikuwa na nguvu sana kiuchumi kisiasa na kitaalamu. Wengine wallimiliki Ardhi kubwa… settlers. Wengina viwanda vikubwa hasa waasia huku wakiwa na uraia wa Waingereza. Ikaonekana wakipewa uraia huku waAfrika wakiwa bado wanapambana na "umaskini maradhi na ujinga" wanaweza wasije ambulia chochote kiuchumi. Watakuta ardhi na rasilimali nyingi zimehodhiwa na waTanzania wakuasili wenye uraia pacha. Ikaamuliwa kuupiga marufuku. Wageni wasifukuzwe lakini wachague kati ya Tanzania na huko walikotoka. Mapinduzi Zanzibar nayo yakaongezea chachu…. raia walioikimbilia nje wakiwa na uraia pacha wangeliweza kusumbua.

Mwalimu Barbro Johanson ni kati ya Wazungu wa TANU walioungana na Mwalimu Nyerere kupigania uhuru yeye akiwa Mbunge wa Kwanza wa Kanda ya Ziwa Magharibi…. yaani Mwanza katika legislative council ambapo kila chama kilitakiwa kuwa na Mwafrika mmoja… Mzungu mmoja na Muhindi mmoja.

Mama Barbro alinieleza kuwa yeye ndiye alipendekeza sera hiyo kwa mwalimu na ikakubaliwa.

Sasa mwaka 1993 aliporejea Sweden akiwa raia wa Tanzania aliomba lakini alinyimwa resident permit ya kuishi Sweden na idara ya uhamiaji kwa sababu aliambiwa Sweden haitambui uraia pacha kwa raia wake. Ukizaliwa raia wa Sweden na ukirudi Sweden automatically wewe ni mswidi umerudi nyumbani. Hayo ya uraia pacha ni adventure zako duniani kulingana na hali yako.

Mama Barbro alifadhaika sana juu ya jambo hili. Alikuwa mzee wa miaka 86. Akamwambia Balozi (wakati huo mme wangu Hayati Wilson Tibaijuka) kwamba atakuja fanya kituko cha ajabu kwa sababu amenyanyaswa na hawezi kusaliti nchi yake Tanzania. Tukahofia kwa utu uzima huo anaweza hata kujinyonga au kukataa kula.

Wakati huo Mama Barbro asingeweza kurudi Tanzania kwa sababu Mwalimu Nyerere alishamuomba asirudi huku Tanzania kwani utaratibu mzuri wa kumtunza haukuwepo. Nilikuwa ninahangaika naye peke yangu nikiwa mwalimu UDSM.

Balozi Tibaijuka alimaliza swala hilo la resident permit ya Mama Barbro kidiplomasia. Wizara ya nchi za nje ya Sweden ikamugongea Mama Barbro 'resident permit" kwenye passport yake ya Tanzania kama alivyotaka lakini kihalisia ilikuwa ni kumtuliza tu. Kwa kifupi kisheria Mama Barbro na wenzake wengi waliojaribu kukana uraia wao hawakufanikiwa. Nchi zao hazikukubali.

Sisi tumevuka mpaka hadi kuwanyanyasa watoto wetu kwa kuwaondolea uraia wao.

NOT RIGHT AT ALL

Kwa sasa tumeelimika. Sababu za miaka 60 kuzuia uraia pacha hazipo tena hasa kwa watoto wanaozaliwa wakiwa raia wa nchi hii. Kumbuka kundi hili kimsingi hawakuwepo miaka hiyo.
Tujielimishe.

Mama Tibaijuka

0 Comment

Leave a Comment