Changamoto za mabadiliko ya mfuko wa bima (NHIF – TOTO AFYA);
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imetangaza kusitisha utaratibu wa matumizi ya Toto Afya Kadi kwa watoto wakiwamo wanafunzi wa Shule ya msingi. Toto Afya Kadi ni kifurushi maalumu ambayo watoto walipatiwa huduma mwaka 1kwa gharama ya Sh50,400/= , BIMA hii ilikuwa mkombozi kwa Watanzania wenye kipato cha chini, gharama ya bima hii ilikuwa nafuu kwa wengi na ni moja ya huduma ambayo ilipokelewa kwa shangwe ya Watanzania walio wengi, lakini kutokana na maboresho mfumo huo umesitishwa. Mabadiliko haya yalitolewa siku ya Jumatatu Machi 13, katika taarifa ya NHIF kwa umma. Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bwana Bernad Konga alisema kama baba hana bima sasa anaruhusiwa kukata ili amjumuishe na mwanawe katika bima hiyo.
Hii ni kasoro ya kwanza, Kwa nini NHIF wanashinikiza Waziza kuwa na BIMA ili watoto wapate bima? Vipi kama mzazi kwa wakati huo hana fedha za kutosha kukata bima yake na ya watoto? Na kwamba angependa kuchukua bila ya watoto kwanza wakati anajipanga kuchukua bila yake? Huduma za afya zinapofanya kwenye mfumo wa kuangalia namna ya kutengeneza wateja ( wazazi kuchukua bima kwanza ndipo watoto wapate bima) Haki ya huduma ya afya kwa watoto imeingia kwenye suala la utata sana, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umetangaza kuwa watoto ambao awali walikuwa wakisajiliwa kupitia utaratibu wa bima ya afya ya ‘Toto Afya kadi, sasa watasajiliwa kupitia vifurushi vya bima ya afya au shule wanazosoma. Ili ni Tatizo la pili, kuna watoto wadogo wengi sana ambao hawajaanza kuingia kwenye masomo, je watakosa bima sababu hawako shule? Hii ina maana gani kwa watoto wachanganya? Kwa nini mfumo huu usiunganishwe na serikali za mtaa na iwe kwa watoto wote.
Kwa nini tunasema mfumo wa kutumia shule unaweza kuwa na changamoto? Je ni watoto wote wanazaliwa wakiwa na uwezo kushiki masomo katika shule? Vipi kama mtoto ana changamoto ambazo awezi kujiunga na masomo katika shule za kawaida na katika umri wa kawaida? Mfumo huu umeleta changamoto ya ubaguzi kwa watoto wengi sana.
Hii inaonyesha wazi kuwa Serikali kupitia wizara husika hawajajipanga, waangalie njia nzuri ya maboresho, kufanya hivi kutapelekea watu wa kipato cha chini kushindwa kumudu gharama za Bima kubwa ambazo zitajumuisha na watoto wao na kupelekea watoto wengi kukosa matibabu.
Taarifa ya NHIF haijaweka bayana kuwa huduma hiyo imesitishwa kwa muda gani, uamuzi huu ni kinyume cha kifungu cha 8 cha Sheria ya Mtoto No 21 ya 2009 ( https://www.lecriconsult.co.tz/files/SHERIA%20YA%20MTOTO%20YA%20MWAKA%2020141.pdf ) kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 ambayo inasisitiza mtoto anapaswa apate haki ya huduma ya afya na kinga katika kustawisha ukuaji wake na pia ibara ya 24 ya mkataba wa Kimataifa wa Haki za mtoto 1989, ambayo inasisitiza haki ya mtoto ya kufurahia kiwango cha juu kinachoweza kufikiwa kiafya na vifaa kwa ajili ya matibabu ya magonjwa na maslahi ya mtoto kwa afya (https://www.ohchr.org/sites/default/files/Documents/ProfessionalInterest/crc.pdf). bara ya 14 ya mkataba wa Afrika wa haki na ustawi wa mtoto 1989 pia inasisitiza kila mtoto ana haki ya kufurahia kupata haki kwa maslahi ya kiafya. ( https://au.int/sites/default/files/treaties/36804-treaty-0014_-_african_charter_on_the_rights_and_welfare_of_the_child_e.pdf )
Kulikuwa na ulazima gani kwa mabadiliko kabla ya NHIF kuwa tayari kuanzisha mfumo mpya? Suala la bima ya afya sio suala la kuvurugwa namna hii, hakuna sababu kubwa zilizopo sasa zilizopeleka uhalaka wa kufanya mabadiliko haya na kuweka watoto wengi katika hatari ya kukosa huduma ya matibabu bila sababu za msingi.
Serikali imemua kukandamiza wazi watoto HAKI yao ya bima ya afya. Kilichofanyika kama mzazi hana uhitaji au uhiari wa kuwa na bima ya afya na mtoto anakosa haki ya kupata bima hiyo jambo ambalo linakwenda kinyume na matakwa ya sheria. Serikali inataka kufanya wananchi wake wawe na maisha magumu zaidi. Bima za afya ni ghali sana na haiendani na hali ya uchumi wa wananchi walio wengi.
Mapendekezo;
- Taarifa ya NHIF iweke bayana kuwa huduma hiyo imesitishwa kwa muda gani na kwa sababu gani. https://drive.google.com/file/d/1QxUaoGb8oX0aoV5Xn16yZopjnXJeAHdL/view?usp=share_link
- Toto Afya Kadi ingeachwa iendelee huku wakiendelea na maboresho mpaka pale watapokuwa na mfumo mpya utaratibu mpya.
- Bima kwa wote izingatie na uchumi au kipato cha mwananchi, kwani maboresho mengi yamefanywa kwa ongezeko la gharama na sio uboreshwaji wa huduma.
- Mfuko wa Bima ya Afya utafute chanzo kingine cha kuwawezesha kuzalisha kipato ili kufikia hadhi ya kuchangiwa kwa kiasi kidogo tu badala ya kutegemea chanzo cha mapato kutoka kwa wananchi pekee kwa ajili ya kuendesha mfuko huo wa Bima ya Afya, kwa sababu serikali ina wajibu wa kutoa huduma kwa jamii.
Athari
- Watoto wengi watakosa huduma ya afya kwa sababu wazazi wengi wanashindwa kumudu gharama za Bima kubwa ambyo inaweza kumjumuisha na mtoto.
Bima ya Afya kwa wote itaathiri upatikanaji wa huduma zingine nyingine kutokana na masharti yaliyowekwa ikiwemo sharti la kutopata huduma nyingine kama leseni, viza, usajili wa wanafunzi mashuleni na vyuoni kama huna bima ya Afya. #ChangeTanzania
Alphonce Dominick
Naunga mkono hoja yako. Mfano sharti la kufikisha kundi la watoto 100 waliolipiwa mashuleni si kila mzazi/ mlezi yupo tayari kumlipia mtoto kutokana na changamoto mbalimbali kama kipato, elimu n.k kujumuisha watoto mashuleni kuna nyima fursa mtoto ambaye angeweza kulipiwa bila kupitia sharti hilo. Pia kwa mtoto mchanga ambaye ndiye yuko kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa (0-5) amewekwa kwenye hatari zaidi kwa kunyimwa haki yake ya msingi ya matibabu. Hii huduma ingerudishwa hadi maboresho mengine yatakapokuwa tayari.