News Details

Je serikali ina nia ya kuleta unafuu kwenye mawasiliano? Hali ya upatikanaji na unafuu wa huduma.

Waziri wa habari, Teknolojia na mawasiliano  Nape Nnauye kipindi cha serikali ya awamu ya 5 aliwasilisha hoja Bungeni ya kuondosha a kurusha matangazo live kwenye televisheni na serikali ikafanikiwa kuyafunga matangazo, hii iliuzunisha wananchi wengi sana, hoja ilikuwa ni kwamba wabunge wengi wanaonge mambo kwa kutafuta sifa, kwamba wanafanya siasa, lakini sasa matangazo live yamerudi, utetezi wa kurudisha ni kwamba TBC zamani ilikuwa inapata hasara kubwa kurusha vipindi hivyo vya bunge, kwamba TBC ilikuwa inapata hasara ya billioni 4 , lakini ni TBC hiyo hiyo ilikuwa inazunguka na Rais Magufuli nchi nzima na kurusha matangazo yao, ila Bunge kama mhimili ikaonekana ni hasara kurusha matangazo yake, Wakati huu tena akiwa na dhamana hiyo hiyo ya Waziri wa habari Teknolojia na mawasiliano ameufungia mtandao maarufu wa Clubhouse. https://drive.google.com/file/d/1_FIrJUmiIf1GCxU_-NBVuoGFC7XJqhzL/view?usp=share_link
Kampuni la kimataifa BlockNet walithibitisha hilo,  alisema wazi kwamba CLUB HOUSE ilikuwa imefungiwa nchini Tanzania, Waziri Nape alijitokeza na kupinga baadaye ya kutoa kauli yake lisaa limoja mbele Club House ikafunguliwa, TCRA wakasema kulikuwa na hitilafu, lakini Club House haiwezi kupata hitilafu Tanzania pekee yake, kwa sababu ana mifumo yake hapa nchini, kama ingekuwa na mifumo hapa nchini ingeweza kueleweka.

Mtandao wa Clubhouse, ni mtandao ambao watu popote pale walipo duniani huingia kujadiliana mada mbalimbali za maisha yao, ikiwemo uchumi, mambo ya kijamii, siasa kwa uwazi na uhuru wa hali ya juu. Mtandao huu  umekuwa ukitumika  kwa kiasi kikubwa kutoa  elimu ya kuwaamsha watu na kuwapatia maarifa makubwa Watanzania, Hii ndio sababu kubwa ya  serikali ya CCM kuogopa na kuona  tishio la mtandao huu,  Mara nyingi serikali imekuwa pambana sana wakosoaji na pia  kukwepa uhuru wa wananchi kuikosoa serikali. https://drive.google.com/file/d/1HUsfb6jtfCUv7MvjNWbhN9zqdN6nkZZN/view?usp=share_link  

Tukumbuke kuwa katika kipindi cha miaka 7 cha kuzuiliwa haki ya kukusanyika ambayo ipo kikatiba wananchi waliona ni vyema kutafuta njia mbadala za kutoa maoni yao na kupata uhuru wa kujieleza ambayo ni pamoja na  mtandao wa club house. Hivyo lengo la kufungia mtandao wa Clubhouse ili Watanzania wasiweze kukusanyika na kujadili mambo muhimu ya nchi yao. Tukumbuke Nape Nnauye ndiye  alikuwa kinara wa kutetea sheria kandamizi ya vyombo vya habari wakati alipokuwa waziri wa habari kipindi cha Magufuli. 

Haiwezekani Rais Samia anasema kuwa anataka kuifungua nchi na uhuru wa maoni uwepo na kukosoa utawala wake ruksa, Lakini Waziri bila kuutarifu Umma anafungia mitandao na pia kwa nini Rais anaonekana kukereka na ukosaoji?. 

Hii mitandao kwa sasa ndio sehemu pekee ya kupaza sauti kutokana na hali mbaya ya watu kupotea mikononi mwa polisi na pia ilitumika  kumtetea Nape Nnauye kipindi kile katolewa bunduki njenje. Je kwa nini serikali haijifunzi? 

Hii si mara ya kwanza kwa mitandao kupata tatizo nchini, iliwahi kutokea hivyo kwa mtandao wa Twitter, muda mchache kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka 2020.

Kuna manufaa mengi kama mitandao ya jamii itatumika vizuri, hutumika kukuza na kutangaza biashara na hivyo wananchi kujipatia kipato. Serikali ilitakiwa kuweka urahisi zaidi katika kutumia mitando hii kwa kuweka unafuu wa bundle na kuhamasisha matumizi sahihi ya mitandao kwa maendeleo ya taifa.

Mfano kutokana na uzinduzi wa mradi wa "Smart Kigali" unaoungwa mkono na serikali, watu nchini Rwanda sasa wanapata intaneti bila malipo kupitia vifaa vinavyowezeshwa na Wi-Fi.

Mradi huo unaoendana na Dira ya 2020 ya Rwanda, unaashiria hatua nyingine ya kufikia matarajio ya taifa hilo la Afrika Mashariki ya kuwa kitovu cha IT kikanda katika mustakabali uliojengwa juu ya uchumi unaotegemea maarifa ili kuvutia uwekezaji zaidi kutoka nje.

Sakata la Starlink

Waziri Nape Nnauye amesema kuwa Kampuni hiyo inayomilikiwa na Elon Musk haijakidhi vigezo ilivyowekewa na serikali ikiwamo kufungua ofisi nchini Tanzania ili waweze kulinda data za watumiaji na kuwajibika kwa watanzania. 

Starlink Wataleta Huduma Ya Internet Kwa Gharama Nafuu Kuliko Ilivyo Sasa kwani gharama za internet nchi zimekua kiasi cha GB 1 kufikia Shiling 3000 kwenye makampuni mengi ya simu. Maeneo mengi hususani vijijini yatanufaika kwani ni maeneo machache ya vijijini ambayo yamefikiwa na mtandao. Itatengeneza ajira, na pesa nyingi kutokana na leseni watakayopewa walitengenezea Taifa pesa nyingi zinazotokana na kodi.

Starlink sasa inapatikana Nigeria Waziri wa Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali, Isa Pantami, alisema kuwa Nigeria imepata asilimia 100 ya mawasiliano ya mtandao wa intaneti kutokana na uzinduzi wa huduma ya satelaiti. Starlink ilipokea leseni za kufanya kazi nchini Nigeria na Msumbiji mwaka jana.

Hatua ya Waziri Nape Nauye hakusema kwanini kampuni ya Starlink kugoma kukubaliana na masharti ya kufungua ofisi pamoja na kuonyesha kwa namna gani watalinda data za wateja wao. 

Hii imezua maswali mengi kwa wananchi mojawapo ikiwa wanahoji kuwa kuna mitandao mingi ya kijamii kama Twitter, Instagram Facebook na mingineyo mbona yenyewe ipo na inatumika kwa wingi nchini na hakuna hata mmoja mwenye ofisi nchini na hatujaona hatua zozote zilizochukuliwa na waziri kuzitaka ziwe na ofisi?

Tukizungumzia suala la wawekezaji kuwa na ofisi nchini serikali imepitisha sheria ngumu ambazo si rahisi mwekezaji ambaye ana lengo la kufanya biashara na kupata faida anaweza kufikiria kua na ofisi nchini, mfano sheria ya kodi ya manunuzi ni 18%, lakini kwa nchi Kama Marekani haijawahi kuzidi 9%, kwa mfano huo mdogo, bado tunahitaji ukarabati madhubuti wa sheria ili kupata wawekezaji na kukuza uchumi wa Tanzania 

#UhuruWaKujieleza #ChangeTanzania

0 Comment

Leave a Comment