Ubovu Wa Miundombinu Ni Changamoto Katika Elimu
Sekta ya elimu ni nyeti katika ukuaji na maendeleo ya nchi. Sekta hii ipo chini ya Wizara ya Elimu. Licha ya kuwa na umuhimu katika Taifa sekta hii inakabiliana na changamoto kadhaa ikiwemo miundombinu bora na vifaa vya kujifunzia wanafunzi, hali ya madarasa sio bora na vitendea kazi kwa walimu na wanafunzi vinakatisha tamaa sana , Vyoo vya shule (Matundu ya choo) bado ni mtihani katika nchi yetu hasa baada ya miaka 61 ya uhuru tumeshindwa kumudu matundu ya vyoo katika shule zetu.
Hivi karibuni tuliona Shule kongwe ya msingi ya Kibeta iliyopo ndani ya Manispaa ya Bukoba yenye jumla ya wanafunzi 967, ikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa madawati , ambapo baadhi ya wanafunzi wanakaa zaidi ya wawili katika dawati moja huku wengine wakikaa sakafuni. https://drive.google.com/file/d/1CxhcWgG0-CMGtgT_Y8u4f5HirJl8jIGS/view?usp=share_link hii ni hali ya kawaida sana katika shule zilizo nyingi.
Shule ya Mvinza Kagerankanda haina madarasa wala madawati. Shule ipo Wilayani Kasulu, Kigoma ina Wanafunzi 2,111, wengi wanasomea nje huku waliopo Darasani wakikaa chini. Madarasa yapo 12, yanahitajika 46 ili kukidhi mahitaji Madawati ni 694 yapo 184 tu. https://drive.google.com/file/d/1UQtJdmi20gEt5aN1zgS7UZrxc4UKiIZm/view?usp=share_link Hii ni mifano bora ya shule duni, watoto wetu wanakosa fursa ya kusoma katika mazingira bora kwa sababu serikali haijaweka kipaumbele, kwa sababu wazazi wameacha suala la elimu na kulitelekeza kwa serikali, wameshindwa kuisukuma serikali kupeleka huduma bora katika maeneo yao, mabadiliko ya kwenye kwenye mfumo wetu wa elimu yatachangiwa na wazazi wenyewe, bila wananchi kuona kwamba tuna dhamana ya kusimamia elimu na tukategemea tu maafisa ya serikali, nchi itaangamia, vipaumbele vya watumishi wa umma vinajulikana ni maslahi yao, ndio maana pamoja na shule kuwa na hali mbaya kama hivi lakini Mkurugenzi wa halmashauri na mkuu wa wilaya lazima watakuwa na V8 na zinajaa mafuta kila mwezi tena kwa matumizi yasiyo na tija au matumizi binafsi.
Shule ya msingi Galigali kuna changamoto nyingi kadiri ya taarifa ya uongozi wa shule Jumla ya Watoto wapo 656 na walimu ni 6 tu. Pia kuna uhaba mkubwa wa madawati watoto kukaa sakafuni ilihali shule yenyewe Ina msitu wa miti ya kutosha. https://twitter.com/lifeofmshaba/status/1627567114964828160?s=20
Tarehe 17 Februari 2023 Madiwani wa halmashauri ya jiji la Mwanza waliiomba serikali itatue changamoto ya upungufu wa madawati, matundu ya vyoo pamoja na madarasa kwa shule za msingi zilizopo katika halmashauri huyo. Diwani wa kata ya Isamilo Charles Nyamasiriri amesema katika shule ya msingi Makongoro kuna matundu sita ya vyoo ambayo hadi sasa hayajaisha wanafunzi wanapata shida ya kujisaidia huku diwani wa kata ya Igoma Musa Ngolo akisema katika shule ya msingi Mandela bado wanafunzi wanakaa chini hakuna madawati.
0 Comment
Leave a Comment