News Details

Tozo Kwa Abiria Na Watumiaji Wa Kituo Cha Mabasi Cha Magufuli.

Moja ya mapato ya Halmashauri au majiji ni tozo kwenye stand za mabasi, tozo ziko za aina nyingi sana, moja ni tozo wanayotozwa abiria wenyewe ticket kuingia kupanda bus, lakini tozo kwa watu wanaosindikiza abiria, na tozo kwa mabus kuingia kwenye stand hizo na tozo kwa wafanyabiashara kwenye eneo la stand.

Hakuna maswali kuhusu tozo za mabasi na wafanyabiashara na pia watu wanaosindikiza abiria, lakini cha ajabu ni TOZO ya mabus na pia kwa abiria, bus limelipa tozo na abiria amelipa tozo hii ni kodi mara mbili kwa abiria, lakini pia nauli aliyotumia abiria tayari kuna tozo au kodi za serikali, hizi ndio zile wataalamu wanasema kodi za kivuli, unategeshea kodi kwenye huduma fulani kutokana na kushindwa kubuni vyanzo vingine vya mapato. Kibaya zaidi TOZO hizi na kodi sio kwa ajili ya maendeleo ya Stand husika, nyingi zinakwenda kutumika kwenye Halmashauri kwa mambo mengine kabisa ikiwemo vikao na safari, na kuacha stand hizi za mabasi zikichakaa, kuwa na huduma mbaya za choo na parking zenye mashimo kwa mabus, lazima mambo mawili yabadilike, moja ni TOZO zote za stand zitumike kwa ajili ya maendeleo ya stand hizo , kutoa huduma ya vyoo na ulinzi, kuboresha hali ya nishati kwenye stand zetu , kwa maana hiyo ndio maana tunasema;  

MFUMO MPYA WA KUINGIA STENDI YA MAGUFULI UNANYONYA WANANCHI.

Jumatatu, February 20, 2023 Manispaa ya Ubungo, ilianzisha utaratibu mpya wa kuingia na kadi katika stendi ya kimataifa ya mabasi ya Magufuli wakisema nia na madhumuni ni kudhibiti upotevu wa mapato kwa abiria wanaoingia katika kituo hicho kilichopo Mbezi Luis. Hakuna hatuna pingamizi na kuanzishwa mfumo wa kadi kwenye malipo, lakini hoja ni fedha hizi zinakwenda wapi? Kuna uwazi kwenye matumizi ya fedha hizi?

Hata hivyo mfumo huu umekosolewa vikali na wananchi mbalimbali kwa kuwa inaonekana kama serikali haikujiandaa kuingia kwenye mfumo huu lakini pia suala la abiria wenye tiketi kulipa ushuru wa kuingia stendi limepingwa vikali na wananchi mbalimbali kwani tiketi hizo tayari zimeshakatwa tozo katika mabasi yanayosafiri kwenda mikoa mbalimbali.  Ticket za mabasi zilitakiwa kuwa na code maalumu ambayo abiria atatumia ili kuingia kwenye standard, au kila Ticket iwe na punguzo sana na tozo za kuingia kwenye stand hizo ili kupunguza mzigo kwa abiria. 

Mawakala wa mabasi pia wamelalamikia utaratibu huo huku wakiomba wapewe vitambulisho maalum vitakavyowaruhusu kulipia mara moja kwani mfumo uliopo unawafanya walipe pesa kila watakapoingia kila wakati hivyo wanajikuta wanatumia pesa nyingi. https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/mawakala-walia-na-kadi-za-kuingia-stendi-ya-magufuli-4131792 

MFUMO WA N-CARD BADO UNA CHANGAMOTO SANA

Mfumo huu wa N-Card umekuja kuumiza pia abiria wengi kuchelewa safari zao na kuachwa na mabasi kwani zipo mashine licha ya upya wake zimekuwa zikisumbua yaani hazifanyi kazi kwa wakati fulani. Hata hivyo madereva wameendelea kulalamika kwamba hata mabasi yanachelewa sana kutoka katika muda husika kutokana na mfumo huo wa N-Card. 

https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/mfumo-mpya-kuingia-stendi-ya-magufuli-walalamikiwa-kuchelewesha-abiria-4133038

Lakini pia hata wanaoutumia mfumo wa N-Card kupitia kivuko cha kigamboni una changamoto kubwa hasa mashine kushindwa kufanya kazi na kusababisha wananchi kuchelewa katika shughuli zao.

Ni vyema serikali ingeangalia upya uwekaji wa mfumo huu, Kwanza kuwaondoa abiria ambao tayari wamekata tiketi zao ili kuepuka kulipa ushuru mara mbi kwani mabasi yanatoa ushuru huo na kila tiketi inakatwa Tozo na serikali. Pia serikali inapawa kuboresha mifumo hiyo ya N-Card ili kusiwe na usumbufu wa kuharibika haribika kila wakati, Na mwisho mawakala wa mabasi watengenezewe vitambulisho maalumu ambavyo vitawasaidia kulipa mara moja pale wanapoingia ili kuepusha gharama ya wao kulipia kila wanapoingia ndani ya stendi ya mabasi ya Magufuli.

#ChangeTanzania

0 Comment

Leave a Comment