Ubadhilifu ukarabati Kivuko cha Kigamboni.
Tarehe 9 January 2023 Kivuko cha MV. KAZI kilirejea eneo la Magogoni Kigamboni kwa ajili ya kutoa huduma baada ya kukamilika kwa ukarabati wake uliogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 4.4 za Kitanzania, Kivuko cha MV. KAZI kiliondolewa kwenye maji baada ya kufikia muda wake wa ukarabati mkubwa na kuanza rasmi kukarabatiwa mwezi Juni mwaka 2022 na mkandarasi Songoro Marine Transport Boatyard katika Yadi yake iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Ikumbukwe kivuko cha MV. KAZI Ujenzi wake umegharimu Shilingi Bilioni 7.3.
Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)Tarehe 19 Februari 2023 imesaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV. MAGOGONI wenye thamani ya shilingi Bilioni 7.5. https://mwanzotv.com/2023/02/16/bilioni-7-kutumika-kukarabati-kivuko-cha-mv-magogoni/ Mkataba huo umesainiwa katika eneo la kivuko cha Magogoni Kigamboni jijini Dar es Salaam kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Lazaro Kilahala na Mkandarasi African Marine and General Engineering Company Ltd ya Mombasa nchini Kenya. MV Magogoni kilinunuliwa kwa Euro 5,287,800 Sawa na Tsh 9.3 billion Mwaka 2008. https://www.temesa.go.tz/news/7-5-billion-set-for-mv-magogoni-ferry-rehabilitation hivyo kuibua maswali mengi inakuwaje MV Magogoni inakarabatiwa kwa gharama sawa na manunuzi yake, TEMESA wanasema gharama za ukarabati wa MV Magogoni ni pamoja na kununua ingini 5, Kivuko hicho kinatumia ingini 4 wanasema kwamba ingini ya 5 itakuwa kama akiba kama moja ya hizo nne italeta matatizo, lakini hakuna ufafanuzi kwamba mchakato wa kubadilisha injini ni mwepesi kwa kiasi gani, na kama mchakato huo wa kubadilisha ingine ni rahisi hapo inaibua swali kwa nini wanapeleka kivuko Mombasa kwa kazi hiyo hiyo? Tunauliza hivyo kwa sababu kuna faida gani ya kununua injini ya akiba kama huwezi wa kuzibadilisha injini hizo tumepeleka kivuko Mombasa kufanyiwa kazi hiyo, kazi ya kubadilisha nchi inachukuwa 75% ya kazi yote inayogharimu billion 7.5
Suala la pili linaloleta utata kuhusu kununu injini 5 badala ya 4, ni je injini zote 4 za sasa zinazosukuma kivuko hicho mpaka Mombasa hazifai tena kwa kutumia kwa miaka 14 tu? Ni sahihi kusema injini za vivuko zinadumu kwa miaka 14 kisha kuondolewa na kutupwa? TEMESA wanaweza kufafanua kuhusu injini za zamani wanakwenda kufanyia kazi gani?
TEMESA pia wameongelea masuala kama mfumo wa umeme na mabadiliko ya mfumo wa uokoaji kwamba wananunua mfumo mpya kutoka India, je ni kweli hatuna mafundi ndani ya TEMESA wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo? Kazi zote ambazo wametoa kwa wakandarasi zisingeweza kufanyika ndani ya TEMESA au nchini kwa bei nafuu na kwa ufanisi? Lakini pia muuzaji wa injini 5 asingeweza kuzifunga yeye mwenyewe kwa bei nafuu zaidi kutokana na injini kununuliwa kwa bei kubwa na nyingi kwa wakati mmoja?
Wananchi walio wengi wamehoji dhana ya ufisadi kushamiri nchini na kwamba haiwezi kuondoka kirahisi kutokana na masuala yenye harufu ya ubadhilifu yanayofanywa na maafisi wa serikali ambayo kwa sasa kwa asilimia 99% ni serikali ya CCM sababu Bunge kama chombo cha usimamizi limefulika wabunge wa chama hicho. Wananchi Walio wengi wamejiuliza ni kwa nini ukarabati unafanyika Kenya , Je nchini hakuna kampuni zenye uwezo wa kufanya shughuli hizo? Tanzania tumezungukwa na bahari, maziwa na mito mikubwa kuliko Kenya, inawezekanaje Kenya kuwa na Kampuni zenye ubora kuliko sisi ambazo kuna eneo kubwa lenye fukwe zinazotumika kwa usafiri?
Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile (Mb) aliliomba Bunge kupitisha azimio la kubinafsisha huduma za vivuko nchini. Dkt Ndugulile alisisitiza kwamba nchini kuna taasisi zenye uwezo wa kukarabati na kujenga meli ndogo ndogo. Hivyo, kufanya ukarabati wa MV Magogoni nje ya nchi, utapelekea kufanya malipo kwa fedha za kigeni na kuathiri ajira ambazo zingetumika kwenye ukarabati huo.
Wananchi ambao ndio walipa kodi pamoja na tozo mbalimbali hawakutamani kusikia kuwa Serikali inataka kukarabati kivuko cha Mv. Magogoni kwa bil.7. wakati bei ya kuunda kivuko kipya ni kati ya bil.8.5 - 9, Kwanini kisingenunuliwa kivuko kipya ambacho kitakuwa bora zaidi ya hiko na kuipatia tenda kampuni ambayo ni mzawa kutengeneza Kivuko hiko kwa wakati huu?
#ChangeTanzania
0 Comment
Leave a Comment