Mifumo Ya Haki Na Sheria Katika Nchi Yetu.
Tanzania tumekuwa na mifumo mibovu ya Haki na Sheria ambayo kwa kiasi kikubwa ina athiri maisha na ustawi wa wananchi katika nyanja zote , Sheria nyingi tulizo nazo na mifumo ina malengo sana na wakati wa mkoloni. Watu wengi hawaelewi kwamba utawala wa sheria sio lazima uwe utawala wa haki au utawala bora, hasa kama sheria hizo zimewekwa zikiwa na malengo kandamizi au kuzuia haki kwa kundi furani katika jamii au jamii yote kwa ujumla, Sheria nyingi tulizo nazo ni kandamizi na zina ukoloni mkubwa ndani yake sababu zina asili hiyo ya ukoloni, kwa maana nyingine kilichotokea tumebadilisha tu rangi ya mkoloni.
.
Hivi karibuni Makamu wa Rais Dr Philip Mpango amekiri wazi kuwa mifumo ya Haki bado ni changamoto kwa kuzingatia matukio yaliyotokea siku za karibuni kuhusu familia moja ambayo kijana wao alipotea kwa mwezi na nusu huku ndugu zake wakikosa msaada wa polisi na baadaye walitangaza msiba wa kijana wao ndipo polisi wakajibu kuwa wanamshikilia kijana huyo ,wako naye hii ni baada ya makamu wa Rais kuingilia kati, je ni watu wangapi wanapotezwa au kutekwa kwa namna hii na wanapotea moja kwa moja kutokana na jeshi la polisi kuwateka na kuwafundia ndani ya kuta za magereza, huu ni sawa na uharifu mwingine, jeshi la polisi linatakiwa kufuata sheria za nchi, mfumo wa ukamataji ni pamoja na muhusika au mtuhumiwa kutoa taarifa kwa ndugu zake kueleza yuko kituo gani na amekamatwa kwa kosa gani, mtu ametekwa na jeshi la polisi mpaka inafikia hatua ndugu wanatangaza msiba ndio jeshi lijitokeze kusema liko naye? , Je kwa nini mifumo hii ina ujasiri wa kwenda kinyume na sheria? Ni kwa faida ya nani? https://drive.google.com/file/d/1CHBYBeqFDmBFTcgcEFJSy95TuwIHRhQy/view?usp=share_link
Jeshi la polisi pia mifumo yake ya utendaji kazi ina mianya inayoruhusu Haki za wananchi kupokwa, Tumesikia Rais anasisitiza kuwepo kwa uvunjivu wa haki za binadamu katika jeshi hilo akasema "Tunataka mifumo yetu isomane, kwamba mtu akikamatwa na jeshi la polisi kisha akitoa maelezo, hayo maelezo DPP ayaone kwake moja kwa moja. Polisi asipate muda wa kuibadilisha, au mtu anawekewa kirungu anaambiwa asaini hapa, tuangalie hilo"- Rais Samia Suluhu
https://drive.google.com/file/d/1jx7TwwxNluFqvTfUBehkzkJt_Ipd9QLP/view?usp=share_link
Lakini swali kubwa linakuja kama Rais naye analalamika kama sisi ni nani atatanzua mifumo hii? Japo ni Rais huyo huyo pia anapinga pinga mchakato wa wananchi kupata #KatibaMpya , Je Rais ana nia ya kweli kuboresha mifumo? Dhamani ya dhati inapimwa vipi kama kauli zinabishana? #KatibaMpya ingeweza kuwa zana nzuri kwa Rais kuweka sawa haya anayolalamikia kama sisi tunavyolalamika, tupate #KatibaMpya kuondokana na huu ukatili wa jeshi la polisi, Kukataa mchakato wa katiba ni sawa na kunufaika na hali ya ukatili wa jeshi hilo, huwezi kataa upatikanaji wa sheria bora bila kuwa mnufaika wa mfumo wa sasa.
Kwa hali ya sasa Taasisi nyingi za serikali zimekosa imani ya wananchi na kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kukosa uadilifu kazi. Mfano Rais alisema akiwa ikulu katika kuzindua Taasisi za mifumo ya haki, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kuna tuhuma za baadhi ya Maafisa kuwategeshea dawa za kulevya Watu wasiokuwa na hatia na kisha kujifanya wanaenda kuwakamata na kuwabambikia kesi.
Hivyo mifumo ya utoaji Haki iliyopo mingi inakinzana na sheria na inapelekea uvunjivu mkubwa wa Haki za Binadamu nchini.
MAPENDEKEZO;
- Kupatikana kwa #KatibaMpya ambayo kwanza itaweka mgawanyo wa madaraka ambao utafanyika kivitendo zaidi kuliko kuainishwa tu kwenye katiba kama ilivyo ya sasa ambapo katiba hiyohiyo inaipa nguvu mamlaka nyingine kuingilia madaraka ya Taasisi nyingine. Mfano katika mhimili wetu wa serikali uningilia sana na mahakama, kama Rais kuteua Majaji hii inaua sana utendaji kazi huru kwa kuwa Jaji anaweza kufanya kazi yake kwa upendeleo au kwa maagizo ya aliyemteua kwa kuhofia kutenguliwa kama akienda kinyume.
- kuwepo na sheria itayoibana mifumo yote ya Taasisi zinazotoa Haki zote kwa ajili ya uwajibikaji na uadilifu katika utoaji Haki na utendaji kazi.
- Iundwe tume huru ambayo wananchi wataweza kwenda kutoa malalamiko yao moja kwa moja au wengine kuwawakilisha kwa vitu kama haki zao zitakandamizwa na serikali au mtu mwingine yoyote.
- Taasisi kama jeshi la polisi kufungwe CCTV CAMERA pamoja na polisi kufungwa kamera mabegani au kwenye kofia zao wanapokuwa kwenye kazi nje ya kituo kwa ajili ya kuzuia matumizi ya nguvu na mateso kwa watuhumiwa ili kuwe na usawa katika utoaji haki na ushughulikiaji wa watuhumiwa kabla ya kufikishwa mahakamani na pia kuwe na mifumo ya kijitali katika kutunza kumbukumbu mara tu mtuhumiwa anapokamatwa ili kuepusha tatizo la watuhumiwa kupotelea mikononi kwa polisi.
- Serikali kupitia #KatibaMpya ilete mfumo ambao utalenga kuimarisha uwajibikaji wa kidemokrasia (uwajibikaji wa kijamii na kisiasa kwa pamoja) katika utoaji wa huduma katika demokrasia zinazoibukia na demokrasia zilizokomaa. Kwa vile demokrasia hasa inahusu udhibiti wa wengi juu ya kufanya maamuzi na usawa wa kisiasa, serikali iandae mbinu itayoruhusu mchakato mpana na shirikishi wa tathmini unaoendeshwa na kumilikiwa na wananchi
- Mfumo wa uwajibishaji pia ni muhimu sana kwa kuwa kuwawajibisha maafisa wa serikali ni kitovu cha Demokrasia. Uwajibikaji wa kidemokrasia unawapa wananchi na wawakilishi wao nafasi na njia ya kutoa maoni yao na kupatiwa maelezo kuhusu utendaji kazi wa maafisa wa kuchaguliwa na wale wasio wa kuchaguliwa, na inapobidi wanashauri hatua za kuchukua kwa maafisa walioshindwa kutekeleza majukumu yao.
- Mabadiliko ya katiba yataweza kusaidia mifumo ya utoaji haki kuongeza uwajibikaji katika utendaji wake kwa kuwa uwajibikaji unapima kiwango ambacho Taasisi hizo katika kuelezea na kuhalalisha maamuzi yake kwa umma. Ufanisi mkubwa wa uwajibikaji unaainishwa kwa namna ambavyo wadai haki wanaelezea mahitaji yao, lakini pia unahusiana na nafasi, uwezo na utayari wa maafisa kuwajibika kwa matendo yao.
Ili kuhakikisha mifumo ya haki na sheria inafanya kazi kwa ufanisi inatakiwa kuwa na usikivu, utekelezaji, uwazi na ushirikishi katika shughuli zake zote na vyote hivyo vitaletwa na #KatibaMpya .
#KatibaMpya #ChangeTanzan
0 Comment
Leave a Comment