News Details

Madaraka Ya Rais Yapunguzwe Katika Suala La Teuzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana madaraka makubwa hasa katika uteuzi ambayo yanapelekea kukwamisha uwajibikaji na utendaji kwa manufaa ya wananchi. Suala la madaraka na majukumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, limezua mvutano katika baadhi ya kamati za Bunge Maalum la Katiba na kusababisha kuziweka kiporo ibara za 72 na 73 za sura ya saba ili kutoa fursa kwa wajumbe kutafakari zaidi.

Mojawapo ya ibara hizo ni ile inayohusu madaraka ya Rais katika uteuzi wa viongozi wa umma, ambayo akitaka anaweza kuchagua hata marafiki zake katika nafasi anazohitaji. Lakini pia hivi sasa tumeona Rais anaweza kuteua watu ili awaondoe katika nafasi fulani kwa malengo maalum, kama ambavyo tumemsikia mwenyekiti wa CWT Bi, Leila Ulaya https://drive.google.com/file/d/1a8P4lEDiRVhaC_aLNFZxJpYTyrRvRyzc/view?usp=share_link

 Rais anahitaji kupunguziwa madaraka kwa sababu;

Kumpunguzia madaraka ina maana ya kumwekea mipaka ya kazi yake na vyombo vya check and balance.

Kumpunguzia madaraka ni kwa lengo la kuwa na serikali inayozingatia katiba, kufanya kazi kwa ushirikiano na vyombo vingine huku kila kimoja kikiwa watch dog ya kingine. Kuwe na check and balance.

Ni katika hiyo check and balance ndipo Rais atakapolazimika kuteua watendaji ambao baada ya kuthibitishwa si wake tena, watawajibika sehemu nyingine. Hii itatoa nafasi za umakini katika kupata viongozi na kumpa Rais ''unafuu'' wa kuwaondoa kwani yeye hatahusika tena.

Hebu fikiria yanayotokea hivi sasa ya watu kugomea teuzi.

Lakini pia kumpunguzia madaraka kunalenga kuongeza ufanisi kwa Rais kwa kumpunguzia kazi zisizo za lazima na zingine zinazomtia katika kashfa. Kwanini Rais wa nchi kubwa kama Tanzania ahangaike na uteuzi wa wakurugenzi wa miji au bodi za mashirika na vyuo?

Kwa ufupi kumpunguzia madaraka Rais haina maana ya kumyang'anya nguvu za kiutawala bali kumpa nguvu za kiutawala kwa kuzingatia, sheria, taratibu na maadili. Ni kumpa uwezo wa kufanya mambo ya kitaifa zaidi, kumwepusha na migongano isiyo ya lazima na vyombo vingine hata wananchi. https://drive.google.com/file/d/1a8P4lEDiRVhaC_aLNFZxJpYTyrRvRyzc/view?usp=share_link

Ni njia ya kumpa nafasi ya kuiangalia nchi kwa ujumla wake na kusimamia majukumu yake. 

Kupunguziwa madaraka kutazuia ''office abuse'' na kumfanya afikirie kwa umakini kila jambo linalogusa wananchi, rasilimali na usalama wao kila sekunde na dakika.

Hatuhitaji kiongozi tunahitaji uongozi na uongozi ambao hautengenezwi na jeshi la mtu mmoja bali collective responsibility ya kila mmoja wetu katika nafasi yake.

Kuna nafasi zilipaswa kuwa za kitaaluma zaidi kuliko uteuzi, hivi karibuni tumeshuhudia wakuu wa wilaya wakiteuliwa wengi wakiwa ni makada wa CCM, hivyo ni wazi kuwa wanaenda kuwa watekelezaji wa maagizo ya Rais kuliko kuwatumikia wananchi . Muhimu ni Rais atambue kuwa yeye ni mtumishi namba moja wa umma na wala si mtumikiwa namba moja.  #ChangeTanzania

0 Comment

Leave a Comment