News Details

Mgogoro wa Ardhi Mbarali Mbeya

Serikali ya awamu ya sita chini ya  Rais Samia imeendelea kutekeleza  uonevu mkubwa na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu katika suala zima la umiliki wa ardhi ( Haki ya kiuchumi)  katika maeneo mbalimbali nchini,  Matukio yalianza huko Arusha eneo la Loliondo na Ngorongoro, kisha kutapakaa kwa kasi maeneno mbalimbali ya nchi, jamii ya Maasai walianza kushughulikiwa  Mapema mwaka 2022.

January 2023, huko mkoani Mbeya,   Mkuu wa mkoa wa Mbeya ametoa taarifa kwa vyombo vya habari akiwa na anapiga marufuku maeneo ambayo chanzo cha mgogoro huu ni upanuzi wa Hifadhi ya Ruaha na kuweka mipaka mwaka 2001. Maeneo hayo yote  yalikuwa yakitumika na wakazi wa mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kilimo. yakijumuisha Eneo la Mnazi , na Madibira Phase 2 ambayo yalikuwa yakitumika kwa shughuli za kilimo ambazo ndizo hutegemewa na wakazi wa Jiji la Mbeya kama nguzo yao ya uchumi.

Lakini Mkuu huyo wa mkoa wa Mbeya alisema yapo maeneo matano 5 ambayo serikali imepiga marufuku kutokana na huruma ya Rais, Wananchi wameachiwa wafanye kilimo kwa wakati huu mpaka mwezi  April 2023 maeneo hayo ni  (LUHANGA, IYALA, KILAMBO , MSANGA)  Wananchi wamepewa notice mpaka mwezi wa nne wahakikishe wameondoka na kuacha kuyatumia na serikali imekiri kwamba imeweka mipaka tayari.

Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka 2022 serikali kupitia Baraza la Mawaziri ilifuta vijiji vyote vitano vya Kata ya Luhanga na vitongoji 47 kutokana na uharibifu wa mazingira pasipo kusikiliza maoni ya wananchi na kuwashirikisha katika uamuzi huo, ujumla eneo la kilimo linaloathirika ni hekta 14 ambalo ni kubwa na litaathiri watu zaidi ya 40,000 wanaojihusisha na kilimo.

Udhaifu wa suala hilo la Rais kuchukua haki za watu za kumiliki ardhi inatokana na ukweli kwamba Sheria zetu za ardhi zimempatia mamlaka makubwa Rais ya kuwa msimamizi mkuu wa ardhi nchini suala ambalo Viongozi wengi hulivunja na kwenda mbali zaidi kwa kupora haki za wananchi pasipo kuwapatia stahiki zao zikiwemo fidia. https://drive.google.com/file/d/1emmOpbRzNkbTP6uVmDxctDtIPf9yoRIe/view?usp=share_link

0 Comment

Leave a Comment