News Details

Je, Rais ameheshimu takwa la katiba kuhusu mikutano ya hadhara kwa nia ya Dhati?

Mnamo tarehe 03 mwezi Januari mwaka 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliruhusu kuendelea kwa mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa amabyo ilizuiliwa na mtangulizi wake hayati Dk John Pombe Magufuli, ikiwa ni takribani miaka 7 bila kuwepo kwa mikutano hiyo. Pamoja na katazo la Magufuli lazima tuweke kumbukumbu kwa usahihi, Rais Samia pia aliweka zuio la mikutano ya vyama vya siasa, akisema ni wakati wa kujenga nchi, kwamba hata nchi nyingine zinapomaliza chaguzi hakua mikutanao ya vyama vya siasa, suala ili sio sahihi, lakini pia ilikuwa ni uvunjifu wa Katiba ya nchi kwa sababu mikutano hiyo ni takwa la kisheria.

Kuna baadhi ya wanasiasa walipata changamoto kutokana na kutotii kauli ya Rais Samia ya kuzuia mikutano ya hadhara, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwa ni mmoja wao, alipokwenda Mwanza kufanya mkutano wa hadhara wa chama chake alitekwa, akapotea kwa siku kadhaa, baadaye polisi walikiri kwamba wako naye na kwenye kufanya ukaguzi nyumbani kwake baada ya siku 3, walichukuwa vifaa kadhaa na alifunguliwa kesi ya Ugaidi chini ya serikali ya Rais Samia, Rais alipoulizwa na BBC kuhusu kesi ya Mbowe alisema kweli ni gaidi na IGP pia alisema Mbowe ni gaidi unaweza kwenda kumuuliza kama ni mkristo mzuri atakuambia ukweli kuhusu ugaidi wake.

Lakini, kutokana na nguvu ya umma serikali ilishindwa kuendelea na kesi ya Mbowe, Rais akajaribu kwa njia nyingi kuonyesha kwamba yeye anajali siasa za ushindani na kuunda kikosa kazi kwa hoja kwamba kitafanya mwafaka wa namna vyama vya siasa vinaweza kuruhusiwa kufanya siasa katika mazingira mazuri, Ukweli ni kwamba hii ilikuwa danganya toto, Rais Samia alikuwa anafanya juhudi kujinasua kwenye ukandamizaji wa demokrasia alioufanya. 

Mwisho tumeona Rais Samia alisema “Uwepo wangu mbele yenu ni kuja kutoa ruhusa kwamba lile tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara sasa linaondoshwa, Wanasema ni haki kwa vyama vya siasa kuendesha mikutano yao ya hadhara lakini ndugu zangu tuna wajibu. Wajibu wetu ni kuwalinda mfanye mikutano yenu kwa salama. Wajibu wenu vyama vya siasa ni kufuata sheria na kanuni zinavyosema.” – Rais Dkt Samia Suluhu Hassan https://www.youtube.com/watch?v=y-3FOjzwdzc

Je Rais Samia anapata wapi mamalaka ya kuruhusu mikutano ya kisiasa? Je ili sio takwa la kikatiba?

Nini kinaendelea sasa !!!

Mambo yalijitokeza baada ya kuruhusiwa kwa mikuatano ya hadhara kwa vyama vya siasa bado imeacha mashaka kama kweli serikali ina nia ya dhati kuendelea kuheshimu katiba na kuvumilia siasa ya vyama vya upinzani.
Kuna mambo yameibuka ambayo yanajenga mashaka sana kuhusu haki hii ya mikutano kwa vyama vya siasa, kuna dalili za ukandamizaji kwa namna au mbinu nyingine zilizoibuka, 

Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Nnauye aliwataka waandishi wa habari kuweka usawa katika uandishi wa habari za mikutano ya hadhara  ya kisiasa ikiwa ni siku chache baada ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kuruhusu mikutano hiyo kuanza kufanyika nchini.

NUKUU : “Ni matumaini yangu kwamba waandishi wa habari mtaweka usawa wa stori zitakazotokana na mikutano hiyo kwa sababu tukibeba hivi hivi tunaweza kupeleka wananchi sehemu mbaya  ambapo habari zingine zinakuwa na matusi uhuru uliotolewa utumike vizuri turekodi yale ambayo yatasaidisha nchi yetu,”  Amesema  Nape Nnauye.

Kauli hii inaonekana kwa watu mbalimbali kama ni kauli ya vitisho kwa vyombo vya habari kutekeleza majukumu yao kwa uhuru zaidi. Kauli hii ni wazi sasa Serikali inashambulia mikutano ya hadhara kwa kupitia vyombo vya habari kwa namna kwamba kuna mambo wanaweza kuruhusiwa na kuna mambo hawaruhusiwi kuonyesha, lakini pia ni kama kutishia vyombo vya habari kwamba sio kila habari utakayoitoa utabaki salama kwa sababu serikali kupitia Waziri wa Habari inaonekana kutofurahi kama chombo cha habari kitarusha mikutano ya vyama vya upinzani live. 

Siku chache baada ya ruhusa hiyo CHADEMA walianza mkutano wao jijini Mwanza ambapo mambo kadhaa yaliyokea ikiwemo kukamatwa kwa waandishi wa habari siku moja kabla ya mkutano wa CHADEMA,  inasemakana waandishi hao walifuatwa na polisi katika ofisi yao jijini Dar es salaam na kupelekwa kituoni, lakini pia waandishi wengine wakiwa njiani kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mkutano huo wa hadhara waliibiwa vifaa vyao vya kazi ikiwemo kamera na vingine. Hii inafanya tuweze kupokea taarifa ya kuruhusiwa kwa mikuatano hiyo kwa tahadhari.

Ni tumaini letu kwamba, huu ni wakati ambao wananchi wote wanapaswa kushikamana na kupigania haki zote za msingi 

#ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi

0 Comment

Leave a Comment