Utunzaji wa maliasili zetu.
Maliasili za Taifa ni kitu kinachopaswa kulindwa na kutunzwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi kwa manufaa ya watanzania wote. Lakini katika nchi yetu maliasili hakuna uwazi katika usimamizi wa maliasili, serikali inachukua mikopo kila siku kuendesha miradi, lakini tuna maliasili za kutosha kama zikisimamia vizuri zinaweza kufanya mambo mengi bila mikopo tunayoona kwa sasa, kwa nini kuna usiri mikataba inayohusu maliasili zetu? Nani ananufaika na maliasili hizi pale mikataba inapofichwa? Kama mambo yako safi kwa nini kunakuwa na siri
Kuna wakati maliasili zetu zimekuwa zikifujwa kwa manufaa ya wageni na watu wachache hasa viongozi bila kushirikisha wananchi, mfano mzuri ni migodi, imekuwa ni machungu kwa wakati wanaoishi karibu na migodi kuliko kupatiwa maendeleo, lakini pia kama Taifa hakuna kikubwa tumepata ukilinganisha na ukubwa wa mashimo tunayoachiwa, athari za mazingira tulizopata, na mbaya zaidi kuna misamaha ya kodi kwenye hizo shughuli, sehemu inapogundulika kuna madini inakuwa mateso kwa wananchi wanaoishi katika hili eneo badala ya kupata manufaa kupitia fidia au uchimbaji wa madini husika.
Lakini pia kama wananchi tuna hili la kujiuliza kuwa, kwanini tukihoji mambo kuhusu usimamiaji wa Maliasili zetu tunaonekana wabaya? Tukihoji tunajibiwa vibaya na uongo na wakati huwa tunajua nini tunachohoji, Hivyo ni wazi tujiulize bila #KatibaMpya je tutaweza kuwa na sauti kwenye maliasili zetu ama tutabaki na maliasili zisizo zetu bali za viongozi wa CCM?
Hivi karibuni tumeona ndege kubwa ya kubebea mizigo iliyoleta utata mkubwa, serikali imeshindwa kutoa vielelezo vya ushahidi wa ndege hiyo ilikuwa imekodiwa na nani, imebeba mizigo gani na ilikwenda wapi, mbaya zaidi pia serikali inasema ndege hiyo ilibeba watalii wakati ni ndege ya mizigo !!! pia uwanja wa ndege KIA kupitia KADCO wanasema ndege ilitua nchi mbalimbali za Afrika, lakini ukiangali record za ndege hiyo kwenye mifumo ya kimataifa , inaonyesha ndege hiyo ilitoka Abu Dhabi na kuja Tanzania kisha ikirudi ilikotoka bila kutua katika nchi nyingine yoyote ile
Imefikia mahali serikali inasema bila wasi kwamba watalii wanakuja nchini wakiwa wamepanda ndege za mizigo kinyume kabisa na sheria za usafiri , inawezekana vipi watalii kutoka uarabuni wanapanda ndege za mizigo halafu ndege zao zinatua kwa siri huko mbugani kusiko kuwa na Uhamiaji wala huduma yoyote zaidi ya kuchimba dawa na kuwinda wanyama na kwanini watumie uwanja wa mbugani usiokuwa rasmi kwa wageni wanaoingia nchini?
Hapa tuna maswali mengi ya kuuliza lakini hata tukihoji au kuuliza tunaambulia majibu ya uongo na yasiyo ya weledi. Kwa mfano msemaji mkuu wa serikali @MsigwaGerson anataka kutuaminisha kwamba moja ya sababu ya watalii hao wa kiarabu kupanda ndege za mizigo ni kwa sababu wanakuja na makontena? https://twitter.com/MsigwaGerson/status/1612169272477769731?s=20&t=YX_SYt1CXTuDCtlRyik9Sw na hayo makontena ni ya kubebea nini? Na pia wanasema kuwa usafirishaji ulisitishwa swali ni je usafirishaji wa Wanyama umesitishwa kuanzia lini na mpaka lini urejee? Kwahiyo tukisema Wanyama wanasafirishwa hatukosei? Je 1502Km2 walizozipora wamaasai Loliondo ni ili kufanya iwe uwanja wa kuwinda na kusafirisha wanyama?
Pia maswali mengine ya kujiuliza kuhusu ndege iliyotua mbugani ni haya
- Tangu lini Watalii wakapanda ndege ya mizigo?
- Watalii gani hawa tusioelezwa walitoka nchi gani na ni akina nani?
- Siku zote tumekuwa tukitangaziwa idadi na kwa picha..... nini kimetokea?
- Kwa nini ndege kubwa ya mizigo itue kwenye viwanja vya ndani ya hifadhi?
- Je ndege hiyo isingeonekana na wananchi serikali ingetoka kutoa taarifa juu ya ujio wake?
Kwa kadri serikali inavyozidi kutoa ufafanuzi usio na tija nd
0 Comment
Leave a Comment