News Details

Rais samia kupinga uanaharakati nchini kwa hoja kuwa ni uadui kwa taifa.

“Tanzania ndio tunaanza mchakato wa Arbitration, Mara nyingi zinafanywa nje Uingereza na kwingine Wanasheria wetu wakifika kule wanakuta mijitu imebobea wanaongea maneno yanatafunwa ndani hawasikii akiangaliwa macho yanakuwa ya bluu au a kijani hiyo scenario peke yake inaanza kumtisha na vifungu vya sheria alivyokwenda navyo vinaanza kuporomoka kwa hiyo kesi nyingi tunazoshtakiwa nje tunashindwa” https://youtu.be/kxpGf9P_WW0 

“Miaka 4 iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo ukweli kilikuwa sio chama cha wanasheria kilikuwa chama cha wanaharakati na mapambano yao yalikua dhidi ya serikali sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikisha wapi? Siwezi kuwashirikisha Mpaka unionyeshe kwamba unanisapoti ndio nitakushirikisha nikikuona una uadui wangu sitokushirikisha utatumia sheria zote za kimataifa na mimi nitatumia sheria za ndani kukuvaa (Kama umekuja na mkono mchafu usinitegeshee nikikuona nitarudi nyuma) kama unataka kufanya kazi na mimi come with clean hands”

“Tulikwenda kwenye magereza mbalimbali nchini tukagundua kwamba wengi wao wana kesi za kubambikiziwa kuna mtu yupo gerezani miaka mitatu haendi mahakamani haulizwi na hakuna kesi ya maaana”



MAONI JUU YA KAULI YA RAIS

Wanaharakati wamekuwa wakipigania haki za binadamu, wakipinga ufisadi na kuibua ukatili wa polisi na vyombo vingine vya serikali.

Wanaharakati wanataka #KatibaMpya ambayo itajenga misingi ya haki nchini. Wakati Mashekhe wa uamsho walipokamatwa na kuwekwa ndani kwa miaka karibu 10 wanaharakati walisema sio sawa na hakuna mtu anatakiwa kukamatwa na kuwekwa ndani bila hukumu ya mahakama, Mashekhe hawa walikuja kuachiwa na serikali ya Rais Samia hii ina maana bila kelele za wanaharakati haki yao ingepotea  sasa iweje ana chuki na watu wa namna hii? Ukingalia kwa makini masuala wanayozungumza na kutetea wanaharakati ni yale yanayogusa maslahi ya wananchi. Rais wa nchi anasimama kwa niaba ya wananchi, sasa kwa nini anashambulia watu ambao wamekuwa wakikosoa na kueleza serikali kupunguza ukatili kupitia jeshi la polisi?

Serikali ya Magufuli ilifunga watu na viongozi wake walikiuka sheria, tumeona Sabaya aliyekuwa DC Hai amekabiliwa na kesi na kukutwa na HATIA, kuna wengi tu wanalalamikiwa na wananchi lakini walau kuna ushahidi kwamba hawa watendaji walikiuka sheria na wanaharakati walikuwa mstari wa mbele kupingana na matendo yao. Kwa nini sasa wachukiwe na RAIS? Kwa nini Rais anaonekana kushindwa kuungana na wapigania haki? 

Kitendo cha kuita wapigania haki kama MAADUI wa Taifa ni hatari na kinatakiwa kukimewa na kila mtu.

#ChangeTanzania

0 Comment

Leave a Comment