News Details

Makala Juu ya adha ya maji inayoendelea nchini.

Changamoto ya upatikanaji wa maji nchini hasa katika jiji la Dar es salaam na maeneo mengine kama Mwanza ambayo ni majiji makubwa  kibiashara imeibua maswali mengi magumu juu ya huduma muhimu nchini, je kuna vipaumbele vya kutosha? Tuna mikakati ya kuboresha huduma hizi na kuzifanya kuwa stahimilivu katika vipindi vyote vya majira ya mwaka ?. Kukosekana kwa maji Serikali haiwezi kuwepa lawama au kuwajibika sababu maji na umeme ni  huduma za msingi lazima ziwe za uhakika, kukosekana kwa huduma hisi uchuchea mazingira ya magonjwa ya kuambukiza lakini pia uathiri kipato cha wananchi hasa  kipato cha chini , kwa kupoteza muda mwingi kutafuta maji na kupoteza biashara maana wengi hutegemea pia huduma hizo katika biashara zao,  Kukosekana kwa ubunifu au matumizi ya sayansi na teknolojia inachangia sana uhaba wa maji au kukosekana umeme, sera ya maji hasa kwa watu wenye majengo makubwa na viwanja kujihudumia sio rafiki , Serikali ingehamasisha uchimbwaji wa visima virefu kwenye viwanda na makazi binafsi yenye watu wengi mafano magorofa imekuwa dhaifu , lakini pia kwa utaratibu wa hifadhi ya maji kwenye mabwawa makubwa ni moja ya sababu iliyotufikisha hapa, lazima kuwe na a utekelezaji mkubwa kwenye hifadhi ya maji 
Wakati jiji la Dar es Salaam lina uhaba mkubwa wa maji, Mkuranga kuna tafiti zinaonyesha kuna maji mengi karibu nusu ya ukubwa wa ziwa victoria, Kwa nini tumeshindwa kutumia maji haya ya ardhini kuhudumia jiji la Dar.

 Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009 imeweka mkazo katika ushirikishaji jamii kwenye utoaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira; na wananchi kupewa fursa ya kuunda vyombo vya watumiaji maji na kuvisajili kwa Msajili ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri husika. https://www.maji.go.tz/uploads/publications/en1547641391-THE%20WATER%20SUPPLY%20%20AND%20SANITATION%20ACT%20NO%2012%20OF%202009.pdf 

Sheria Na.5 ya mwaka 2019 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira, pamoja na mambo mengine, ilianzisha Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ambayo ilichukua majukumu yaliyokuwa hapo awali yamekabidhiwa kwa OR-TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa (RSs) na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Majukumu yaliyohamishwa ni pamoja na kuhakikisha huduma za maji zinapatikana kwenye jamii za watu waishio maeneo ya vijijini, miji midogo na Makao Makuu ya Wilaya.

Pamoja na hilo, Sheria Na.5 ya mwaka 2019 imehamisha uwajibikaji wa maafisa wanaohusika na utoaji wa huduma ya maji kutoka OR-TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa (RSs) na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenda Wizara ya Maji. Wakala mpya iliyoanzishwa (RUWASA) ina ofisi ngazi za Makao Makuu Dodoma, Mikoa na Wilaya. Hii ni tofauti na muundo wa hapo awali ambao ulikuwa unajumuisha ofisi katika ngazi ya Serikali za Mitaa (LGAs) na Sekretarieti za mikoa (RSs). Lakini pamoja na uwepo wa sheria na mabadilko hayo hakuna matokeo chnya katika upatikanaji wa huduma ya maji, Je shida ni nini kwa nini hakuna uwajibikaji na uwajibishwaji katika eneo hili? 

Katika jiji la Dar Es Salaam hivi karibuni kumekuwa na uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali kusababisha kero kwa wananchi na usumbufu mkubwa kwa wakazi wa Dar Es Salaam na kukosa huduma hiyo muhimu kwa afya ya binadamu, kwa kuwa sote tunajua kuwa maji ni uhai. https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/makalla-atangaza-mgawo-wa-maji-dar-3997512 

Kwa mujibu wa taarifa za mamlaka ni kwamba kiwango cha uzalishaji maji katika mitambo ya Ruvu juu na chini inayotumika kusambaza maji katika jiji hilo na maeneo ya Pwani kimepungua kutoka lita milioni 466 kwa siku mpaka 300. Hali hii inakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tangu Mamkala ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) itoe tathimini yake ikisema jiji hilo linajitosheleza kwa maji kwa karibu asilimia 96. Kulikoni sasa?

Kwa taarifa kama hizo bado kunaonekana kuna opotoshaji  mkubwa kwenye taarifa zinazotolewa na viongozi wa serikali juu ya miradi mikubwa  ya maji , Majanga yanapo ibuka kama hivi tunavyoona upungufu mkubwa wa maji ndipo wanajitokeza tena kupoza wananchi na kuandaa uongo mwingine wa kuendelea kutuliza  wananchi, lakini uhalisia ni kwamba wanaoteseka ni wananchi . 

Ni wazi kuwa tatizo la maji nchini linachangiwa na ukosefu wa miundombinu ya kuwapatia Watanzania maji safi na salama HAKUNA hifadhi ya maji ambayo ingeweza tumika kwa miezi kadhaa inapotokea dharura au maafa, utamaduni wa kuhifadhi maji sio kipaumbele kwa mamlaka husika, hawatoi elimu wale kukaribisha technologia ya uhifadhi maji majumbani. Tumekuwa na miradi chefuchefu  iliyo chini ya kiwango ambayo inahitaji marekebisho mara kwa mara na inapelekea adha kubwa kwa wananchi, Bomba linalopita TEGETA toka Ruvu mpaka chuo kikuu eneo la Makongo tulitegemea lingekuwa na ukombozi, lakini je kuna hifadhi ya maji ya kutosha kwenye eneo husika? . Tanzania imebarikiwa vyanzo vya maji vya kutosha ni aibu kubwa kulia na mgao wa maji au maji kukosekana kwa kuwa tu serikali imeshindwa jambo dogo tu la kusimamia zoezi zima la kuwafikishia maji watanzania.

Kwa mujibu wa DAWASA, hatua za sasa za muda mfupi, mradi wa kigamboni utakua msaada ukitarajia kupunguza uhaba wa maji hasa katika wilaya za Ilala na Kigamboni.Kwa mujibu wa wizara ya maji walisema kuwa mradi huu ungekamilika April 2021 na kuanza kuwanufaisha wakazi wa kigamboni na mji mzima wa DSM, Je changamoto ni nini mpaka sasa mradi huo haujakamilika na wananchi wanapata adha kubwa ya maji?.

Wakati tukiendelea kusubiri kina cha maji kiongezeke kwenye mitambo yake kwa "kudra za mvua" mambo mengine ambayo yanatajwa kufanywa na Dawasa sasa ni kutumia visima virefu zaidi ya 170 vilivyopo ambavyo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amepanga kuvitembelea.

#ChangeTanzania

0 Comment

Leave a Comment