Utawala wa sheria Loliondo na Ngorongoro
Leo nitazungumza kuhusu sheria uhifadhi ya wanyama pori ya mwaka 2009 ambayo kwayo hii amri ya kutenga maeneo mawili ya wilaya ya Ngorongoro yaliyopo katika eneo la Loliondo kuwa ni maeneo ya udhibiti wa wanyama pori, sio mapori tengefu ya wanyapori, nitaelezea tofauti kati ya haya maneno mawili.
Kwasababu yana umuhimu mkubwa sana na baadae swali ambalo najiuliza nitataka kulijibu ni kwamba ‘Hili tangazo la haya maeneo mawili ya Loliondo kuwa maeneo ya udhibiti ya wanyamapori ni halali au ni hamaramu kama kawaida ya mambo ya Tanzania ya CCM.
Nikiuliza swali hilo nahisi wengi mnajua jibu langu ya kwamba, kilichotangazwa ni haramu tupu kwa mujibu wa sheria ya wanyama pori, mkihisi hivyo mtakua hamjanikosea. Kwanza nianze kwa kusema yale ambayo ni fact zisizokuwa na mgogoro wowote yaani yale ambayo hayana ubishani, hakuna ubishani sasa kwasababu tuna ushahidi sasa kwamba wiki iliyopita tarehe 17 ya mwezi huu waziri wa maliasili na utalii na maliasili, Mh Pindi Chana ametoa amri inayoitwa amri ya kutangaza eneo la udhibiti wa wanyamapori linaloitwa POLORETI Haya maeneo mwili yaliotengwa kwa ujumla yake yanaitwa POLORETI GAME CONTROL AREA
Haya maeneo mawili kwa ujumla wake limetangazwa tarehe 17 June ya mwaka huu yani wiki iliyopita na limetangaza kisheria kwa kuchapishwa kwa gazeti la serikali linaloitwa namba 221 la 17 June 2022 hili halina ubishi.
Kuna kitu kingine hakina ubishi kwamba kwa mujibu wa tangazo hili eneo ambalo limetengwa lina ukubwa wa km za mraba 1952. Tumekuwa tukiambiwa na waziri mkuu na hili ni muhimu kwa sababu waziri mkuu wetu ni muongo, sasa waziri mkuu wetu na serikali nzima wametuambia eneo linalotengwa ni km za mraba 1500 ukweli usiokuwa na shaka na ushahidi wake ni tangazo lenyewe ni kwamba eneo linalochukuliwa ni km 1952.
Kuna KM 1502 za mraba za eneo la kwanza ambalo linapakana na hifadhi ya serengeti, kun aeneo la pili ambalo hawalisemi kabisa lipo chini mwa Lake Natron, eneo unalolipita ukienda Loliondo hili eneo lina ukubwa wa km 450 kwa hiyo jumla ya eneo lote ambalo zilizotangazwa ni km 1952 na sio km 1500 ambazo tumeaminishwa, na serikali ya uongo ambayo inasema Rais Magufuli anafanya kazi ofisini kumbe amekufa huo ni uongo.
Na mpaka sasa sijui ni kwanini Rais Samia anasubri nini kumfukuza kazi Kasimu Majaliwa, mtu ambaye anaidharaulisha serikali nzima na chama kwa uongo. La tatu ni kwamba hili eneo ni eneo la udhibiti wa wanyama pori sio eneo tengefu la wanyapori, kisheria hili eneo sio game reserve bali ni game control area, maana ya kuwa game control na game reserve ni nini? eneo tengefu la wanyapori ni eneo ambalo linatangazwa na Rais kwa kushauriana na halmashauri za serikali za mitaa wa maeneo husika na kutangazwa kwenye gazeti la serikali, eneo la udhibiti linatangazwa na waziri baada ya kushauriana na halmashauri za serikali za mitaa wa maeneo husika.
Hili lililotangazawa ni Eneo la udhibiti wa wanyamapori, tofauti muhimu zaidi ni kwamba ukitangaza eneo kuwa eneo tengefu la wanyama pori kwa mujibu wa sheria eneo hilo linaondolewa mikononi mwa wananchi na ndio maana katika sheria ya wanyamapori imelekeza kwamba eneo likitangazwa kuwa game reserve ni lazima wananchi walipwe fidia ya haki na kutekelezwa na sheria imesema iwalipe fidia kwa mujibu wa sheria za ardhi, mpaka kufanya tathmini na kulipwa fidia ya haki timilifu na ya wakati muafaka. Kwenye Maeneo ya udhibiti kwenye haya maeneo ambayo yametangazwa sasa, hakuna masharti yoyote ya kulipa mtu fidia, swali ni kwanini. Jibu lake ni kwamba sheria hii imepiga marufuku kutangaza eneo la ardhi ya vijiji, unaweza kutangaza katika eneo ambalo sio ardhi ya vijiji tu.
Kwa waliomsikiliza mbunge wa Ngorongoro jana amenikosha sana amezungumza hoja nzuri sana na mwenye mawasiliano yao anifikishie pongezi zangu. Hoja ya mbunge wa Ngorongoro jana ni kwamba hilo eneo mnaloliita eneo tengefu ni eneo la vijiji kwa hiyo huwezi ukatangaza Maeneo ya udhibiti kwenye eneo la vijiji. Kuna vijiji zaidi ya 14 na watu tumewaona kwenye picha sasa kilichofanywa na Dkt Pindi Chana na ninaambiwa ana PHD ya Sheria, Miaka kumi iliyopita kuna siku nilisema “Waliozoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi, walio zoea kufanya haramu halali hawaiwezi”.
Wamekuwa wanasema waziri mkuu muongo, tulikua na waziri anaitwa Sospeter Muhongo sasa tuna waziri mkuu anaitwa Majaliwa Muongo. Waziri mkuu na wapambe wake wote waliounga mkono haya ya Serikali ya huyu anayeitwa mama, wengi wanasema hili eneo linatengwa kwa ajili ya uhifadhi sasa hoja yangu ya nne ni kwamba hakuna uhifadhi wowote ule eneo hili linatengwa kwa ajili ya uwindaji, Kwenye maeneo yaliyotengwa kama game reserve au kama Maeneo ya udhibiti moja ufugaji umepigwa marufuku iwe ni kwenye Maeneo tengefu ya wanyama pori au Maeneo ya udhibiti. Kumbuka kwenye Maeneo tengefu ya wanyama pori watu wanalipwa fidia na wanaondoka na hawawezi kutangaza katika eneo la vijiji peke yake kwa maana hiyo watu hawawezi kwenda kuchunga kwasababu sio eneo lao.
Kwahiyo katika maeneo yote mawili kuchunga wanyama kumepigwa marufuku, kwenye maeneo tengefu ya wanyamapori imepigwa marufuku kabisa na kwenye Maeneo ya udhibiti ni marufuku mpaka upate kibali cha maandishi kwa mkurugenzi wa wanyama pori kwahiyo mmasai akitaka kuchunga ni lazima aende Dar es salaam au Dodoma kwenye ofisi ya mkurugenzi wa wanyamapori kuomba kibali.
Hata hivyo uwindaji kwa mujibu wa kifungo cha 20 (2) uchomaji, kukamata wanyama, kuua, kujeruhi, kuvua samaki imeruhusiwa kama umepata leseni ya mkurugenzi wa wanyama pori, haya maeneo mawili wamesema yametengwa kwa ajili ya uhifadhi ni uongo yametengwa kwa ajili ya uwindaji.
Kwa Sababu sheria inasema uwindaji uchomaji, kukamata wanyama, kuua wanyama, kujeruhi, au kusumbua wanyama au samaki inaruhusiwa kama umepata kibali cha mkurugenzi wa wanyama pori na serikali yao ndio wanafanya biashara kubwa na makampuni yanayokuja kuwinda ya kitalii kwa kutumia vifungu hivi, kwahiyo haya maeneo mawili yamepokonywa kwa wananchi ili yagaiwe kwa wawindaji wa kitalii sio kwa ajili ya kutengwa kwa uhifadhi.
Kulikuwa na maneno mengine kwamba haya ni mazalia ya wanyama hii habari nayo ni ya uongo kwa sababu maeneo yanayotengwa kwa ajili ya mazalia ya wanyama yanaitwa “Breeding and disposal area” kwenye sheria na utaratibu wa kuyatenga upo tofauti na huu ambao amezungumza huyu waziri wa sheria Dkt Pindi Chana. Kwahiyo hayajatengwa kwa ajili ya mazalia ya wanyama bali uwindaji kwasababu ni maeneo yanayoruhusu uwindaji, kuua wanyama kujereuhi wanyama na kusumbua wanyama au samaki.
Vile vile haya ni maeneo ambayo endapo kukagundulika madini yanaweza kutengwa kwa ajili ya uchimbaji wa madini kwasababu sheria imesema maeneo haya uchimbaji wa mafuta, gesi asilia, au urani unaruhusiwa baada ya kufanyika kwa masharti ya kimazingira na taratibu nyingine kama kulipa ushuru.
Kumbukeni kwa wale wafatiliaji wa madini moja ya maeneo yaliyogundulika kuna madini ya oil exploration ni bonde la Natron na hizi km 450 za maeneo haya kuna eneo la magharibi linalopakana na Serengeti national park na eneo la mashariki linalokaribia Lake Natron, nafikiri litakuwa sehemu ya lake Natron ambalo ni eneo mojawapo lililotengwa kwa ajili ya oil exploration block kwa taarifa zangu za miaka ya nyuma Lake Natron ni eneo ambalo lilitengwa na TPDC.
Waziri wa maliasili na utalii alipewa mamlaka ya kutangaza maeneo ambayo zamani yalikuwa ni game Control Area kwa sheria ya 1951 kama ilivyobadilishwa na sheria 1974, anataka yaendelee kuwa Game Control Area. Kabla ya sheria hii ya sasa kutungwa sheria iliyokuwa inatumika ni ya mwaka 1974 (Wildlife conservation Areas act ) Na kabla ya mwaka 1974 sheria iliyokuwa inaitwa FAUNA PROTECTION ORDINANCE, Kwahiyo haya maeneo yamekuwa Game Control Area yakayuhishwa na wakoloni mpaka mwaka 1974 na yakaendelea kuwa Game Control Area mpaka 2009.
Ilipotungwa sheria ya sasa kwenye kifungu cha 16 inasema waziri anatakiwa atangaze ni maeneo gani yaliyokuwa Game Control Areas anataka yaendelea kuwa hivyo. Kwa hiyo hakukuwa na muendelezo wa haya maneno, kuna mbunge mmoja alizungumza alisema kwamba haya maeneo yalikuwa Game Control Area toka 1951 chini ya sheria ya fauna, na yakaacha kuwa Game Control Area mwaka 2009 kwasababu sheria hii mpya ilimtaka waziri ndani ya mwaka mmoja tu ya kutangaza kuwa ni maeneo yapi anataka yaendeleee kuwa Game Control Area, alipewa mwaka mmoja tu. Sasa waziri ametangaza hili eneo wiki iliyopita yaani miaka 12 baada ya muda wa kutangaza kupita, sasa kwenye sheria zetu za ardhi ukinyanganywa ardhi miaka 12 usiipoidai sio ya kwako tena.
Waziri alipewa mwaka mmoja tu akalalia haki yake kwa miaka 12 imekula kwake, alichokifanya wiki iliyopita ni haramu tupu na hana mamlaka ya kutangaza eneo kuwa Game Control Area. Kwa mamlaka aliyopewa mwaka 2009 na hana mamlaka ya kutangaza maneno ya ardhi ya vijiji kuwa Game Control Area, walizoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi, waliozoea vya haramu vya halali hawaviwezi, hii ni serikali ya kunyonganyonga tu, ushahidi ni huu hapo sijauliza kwamba kulifanyika mashauriano kati ya waziri na halmashauri ya vijiji kuhusu hayo makubaliano kwa vile wamewakamata viongozi wa vijiji nahisi hakukuwa na mashaurinao nao.
Naomba nipendekeze jambo la haraka sana, nawaombeni sana tafuteni watu (wananchi) waliopo katika hilo eneo kupendekeza maombi ya Judicial Review yapelekwe mahakama kuu kanda ya Arusha, mkaombe amri ya mahakama ya Certiorari kufuta hili tangazo la waziri kwa hoja ya kwamba Waziri hana mamlaka ya kutangaza haya maeneo kuwa Game Control Area, Kwa Sababu ni ardhi ya vijiji na pili mamlaka yake yaliisha mwaka 2009 kwa sababu mamlaka yake yalikua ya mwaka mmoja tu na yaliiisha mwaka 2010.
Hili tangazo kwa jinsi nilivyo fundishwa na Profesa shivji na marehemu prof, Mwaikusa ni kwamba hili Tangazo la Dr Pindi Chana mwenyekiti wangu wa amani wa kamati ya sheria na katiba bungeni ni tangazo ambalo ni ULTRA VIRES Wildlife Conservation Area act, Ni tangazo lililotungwa nje ya mamlaka ya sheria ya wanyamapori.
Pelekeni hiyo application ya judicial review na tuta piga kelele kweli kweli ili Majaji wajue kwamba tunaangalia kwa macho yote kwa chochote watakachofanya, kisheria tu hili tangazo haliwezi kudumu nusu saa kwa hoja za Kibatala na Mtobesya na timu yao. Kwahiyo nawaombeni sana wanasheria wa Ngorongoro na vijana mnaonisikiliza kwa sababu ni ardhi yenu jitokezni muwe wadai katika hiyo hiyo application itakayopelekwa Arusha kusikilizwa.
#StopMaasaiEviction #ChangeTanzania
0 Comment
Leave a Comment