News Details

Makala Juu ya Yanayoendelea Ngorongoro.

Changamoto katika maneno ya uhifadhi ni za muda mrefu sana, Ngorongoro ni moja ya eneo ambalo limekuwa na matatizo hayo. Kwa ujumla mahali popote ambapo kuna maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya uhifadhi ukienda  ndani yake au pembeni yake kuna migogoro mikubwa.  Japo sheria ziko wazi kuhusu shughuli za binadamu na haki ya wana vijiji wa maeneo hayo kwamba wapewa kipaumbele dhidi ya wananyama, lakini uzoefu unaonyesha tofauti ni kwamba serikali imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wanyama dhidi ya binadamu pale mgogoro unapozuka, mbaya zaidi ni ili suala jipya toka miaka ya 1992 ambapo wawekezaji upewa kipaumbele zaidi kuliwa wananchi wa eneo husika, Loliondo ni mfano nzuri kwa uzoefu huu.

Nchi yetu theluthi moja ya ardhi yake  iko katika eneo la uhifadhi, hata hivyo matatizo mbalimbali ya kihifadhi ni janga la la muda mrefu na wananchi katika makazi hayo wanakumbana na changamoto mbalimbali zinazopelekea kukandamizwa kwa haki zao za msingi.

Kihistoria Mgogoro wa Loliondo ulianza mwaka 1954 japo kuanzia 1951 kulikuwa na mvutano sana kutoka kwa mashirika ya kigeni ya kikoloni ambayo yalihitaji wananchi wafukuzwe katika hifadhi ili liwe eneo kwa ajili ya utalii.

Hivi karibuni Kwa maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisema Loliondo ni mali ya serikali toka mwaka 1951 kwa ajili ya uhifadhi lakini  kuna kesi mahamani, kuna zuio la mahakama mpaka msingi itakapofanyiwa maamuzi, serikali imevamia na kuchukua 1500 ambayo ni sehemu ya 4000 za mgogoro. “Tunaendelea na zoezi la kuweka mipaka katika eneo la pori tengefu la loliondo ambalo ni km za mraba 1500, na kwa mujibu wa sheria ni km za mraba 4000” Alisema mkuu wa mkoa wa Arusha.

Tarehe 10 juni 2022, msafara wa magari ya polisi zaidi ya 50 yalikwenda Loliondo na siku iliyofata polisi hao waliwavamia wakazi wa maeneo hayo na kuwapiga, na kuwajeruhi na kupelekea kifo cha askari mmoja wa Jeshi la Polisi. https://www.youtube.com/watch?v=51QkVBjQKaM  

Wakati haya yanayoendelea kumeibuka mijadala mbalimbali juu ya chanzo cha migogoro hii inayotokea ndani ya hifadhi hizi.

Wakazi mbalimbali wa maeneo ya Loliondo wamekiri wazi kwamba serikali inahitaji kuanzisha Loliondo kama Game Control na hili ni jambo ambalo limeanza kwa muda mrefu pasipo mafanikio katika maeneo hayo. 

Mwaka 1951 zilitangazwa hifadhi nyingi kuwa game control ares lakini Loliondo haikuwa mojawapo kati ya hizo zilizotangazwa. Hata hivyo ili hifadhi ipitishwe kuwa Eneo la pori tengefu kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi, Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na serikali ya mtaa, baraza la madiwani wanatakiwa wapitie upya kisha watangaze hizo game control ambazo zina sifa husika Na sifa mojawapo isiwe ardhi ya vijiji. Kwa sasa Loliondo ni Ardhi ya vijiji kwa mantiki hiyo basi kinachofanyika kwa muda huu ni kuwaondoa watu ili ibaki ardhi tupu bila binadamu iweze  kukidhi kuwa Game Control area.

Makundi mengi yamekuwa ya kishambuliwa kuhusu kuongelea na kutoa taarifa juu yanayoendelea Loliondo. Na serikali imekuwa ikipotosha na kusema hakuna jambo lolote linaloendelea Ngorongoro na kuwa kuna amani na utulivu na haya yalithibitishwa na Waziri mkuu bungeni Tarehe 10 June 2022 https://www.youtube.com/watch?v=hRmE1vebmoI  na Spika wa Bunge akawaonya watu wanaotuma taarifa mtandaoni juu yanayoendelea Loliondo na akaagiza wachukuliwe hatua. https://www.youtube.com/watch?v=1UwqWxos3pw 

Na hata hivyo Serikali kupitia mabalozi wake katika nchi mbalimbali wamekuwa wakipotosha wazi juu ya ukweli unaoendelea katika maeneo hayo ya Loliondo.

Hata hivyo makundi ya viongozi wakiwemo Wabunge 3 wa CCM akiwemo mbunge wa Ngorongoro,Emmanuel Oleshangai,Prof Kitila Mkumbo na Christopher Ole Sendeka walihojiwa na polisi kwa tuhuma za Kufanya uchochezi,kupanga njama na wananchi wasitii maagizo ya Serikali Loliondo. 

Ambapo Tarehe 15 June 2022 Mbunge Kitila Mkumbo alithibitisha kuwa yupo salama baada ya kuhojiwa na vyombo vya ulinzi na usalama. 

“Tarehe 6 mwezi June, 2022  watendaji katika mamlaka za ngorongoro wote waliitwa Karatu kisha wakaambiwa waje na mihuri, kuna watu wanadhani watatumia watendaji wa vijiji kwenda mahakamani kwahiyo wanawapora  mihuri” Mkazi wa Loliondo Joseph Oleshangay Aliongezea katika Mjadala wa #MariaSpace katika mtandao wa Twitter.

#StopMaasaiEviction #ChangeTanzania 

Hata hivyo balozi mbalimbali zimekuwa zikihoji juu ya machafuko yanayoendelea Loliondo ambapo Tarehe 16 Juni 2022 Balozi wa Marekani Nchini alikuwa na kikao na Waziri mkuu kujadili masuala yanayoendelea Loliondo  Mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yamepinga vikali juu ya suala la kuhamishwa na kunyanyaswa kwa wananchi wa loliondo, Amnesty International kupitia Deprose Muchena, ambaye ni mkurugenzi wa shirika hilo kwa ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika alisema “Uhamisho huu wa kulazimishwa usio halali unashtua katika kiwango chake na ukatili wake. Mamlaka za Tanzania hazipaswi kamwe kutenga eneo hili kwa biashara ya kibinafsi bila kwanza kushauriana na jamii ya Wamasai, ambao maisha yao yanategemea ardhi ya mababu zao. Iwapo unyakuzi huu wa ardhi utaendelea, maisha na njia ya maisha ya jamii ya Wamasai iko hatarini,” https://www.amnesty.org/en/latest/news/2022/06/tanzania-halt-brutal-security-operation-in-loliondo/ 

 

 

Umoja wa mataifa (UN) umeitaka serikali kuondoa maafisa wake wa usalama Loliondo ili kukomesha ukiukwaji wa haki za binadamu na unyanyasaji unaodaiwa kufanyika katika eneo hilo ili kuruhusu waandishi wa habari, wanasheria, waangalizi wa haki za binadamu na asasi za kiraia kuingia Loliondo, kuzungumza na Wamasai walioathirika na kuripoti hali hiyo bila vitisho.

 

   

0 Comment

Leave a Comment