Sakata la Kupotea kwa wakili Peter Madeleka.
Kuna taarifa za kuaminika za kutekwa kwa mwanasheria Peter Madeleka alipokuwa akitoka Serena hotel. Taarifa kutoka kwa wakili wake (ambaye mpaka sasa ajaonana na mteja wake) zinasema Madeleka aliitwa na watu waliokuwa wamesimama pembeni ya gari hapo Serena Hotel, alipokwenda kuwasikiliza walimshinikiza kuingia kwenye gari ambayo haikuwa na namba zozote ( gari hili haijulikani ilikuwaje likaruhusiwa kwa maegesho ya hotel ya kimataifa kama serena). Je Hotel ilikuwa inajua huu mkakati wa utekaji ambao haukuwa na hati ya mashitaka lakini wakaruhusu tukio kufanyika kwenye eneo la hotel? Walijiridhisha vipi kwamba hao walikuwa ni maafisa wa serikali ? Inakuwaje kwenye hotel yenye wageni magari na watu wasio na sare za kazi wanaruhusiwa kuendesha operation zao za giza?
Baada ya muda Peter Madeleka alipiga simu kueleza kwamba yuko Wizara ya Mambo ya Ndani amekamatwa na kupelekwa hapo. Mwanasheria wake alikwenda hapo wizarani akiwa na dawa lakini hakufanikiwa kumuona kutokana na kuzungushwa sana na maafisa wa polisi. Baadaye aliambiwa aondoke mteja wake yuko salama na kesho yake asubuhi alielezewa kwamba ingekuwa sawa kwenda kumuona, Wakili wa Madeleka alipofika hapo asubuhi hiyo maafisa wa polisi kwanza walisema hawana cha kusema lakini labda bosi wao wa mambo ya makosa ya mitandao, walipokwenda kumuona alisema hana taarifa atafutatilia wakapeana namba za simu kwa mawasiliano. Waliposhuka chini na kuuliza wale askari wakajibu kwamba walichanganya jina mtu waliyenaye sio Peter Madeleka, Wanasheria waliposema huyo Peter waliyenaye ni sawa wawapeleke watamwakilisha hata huyo, polisi walikosa majibu na kukataa kuwapa ushirikiano wowote.
Baada ya kelele mtandao polisi walisema wako naye katika kituo cha Kikuu cha Polisi Dar es salaam, kwamba anashikiriwa kwa kwa makosa ya kutuhumu Jeshi la Uhamiaji kutaka kufanya jaribio la kumuua. Hii ni kutokana na yeye kuendesha mjadala wa namna VIZA fake zinavyotolewa na jeshi hilo katika viwanja vya ndege. Madeleka alitweet na kusema group la Whatsapp la maafisa wa uhamiaji linafanya mikakati hiyo, badala ya kupata ulinzi amekamatwa kwa kosa la kusema usalama wake uko hatarini. Pamoja na kwamba ameshikiliwa na Jeshi la Polisi (ukamataji ukiwa umefanywa kwa namna ya kuteka ) mpaka sasa hakuna kituo cha polisi kimekiri kufanya tukio hilo, lakini pia Jeshi la polisi liko kimya wakati masaa 48 yakiwa yamepita ambapo kisheria hii ni sawa na mtu mzima kupotea kama hajapatikana kwa masaa 48.
Kulikuwa na taarifa kutoka kwa wanafamilia kwamba polisi wamezunguka nyumba yake huko Arusha na baadaye kufika kwenye ofisi yake hapo Arusha kwa ukaguzi. Mpaka sasa Jeshi hili halijatoa taarifa rasmi ni nini hasa wanatafuta au kukiri kwamba wamemshilikia Madeleka.
Serikali ya awamu ya sita inajipambanua kinyume na matendo kama haya lakini chini kwa chini yanafanyika na vyombo vya ulinzi na usalama kuficha taarifa, polisi wanapokamata mtu kinyume na taratibu ni utekaji na ni kosa la jinai, hakuna afisa wa serikali kwenye ofisi yoyote ile ana haki ya kufanya utekaji.
Madeleka aliwahi kuwa afisa katika jeshi la polisi, ni mtu mwenye ufahamu na weledi wa mambo ya VIZA na namna mifumo imekuwa ikichezewa, kitendo cha kukamatwa kwake baada ya yeye kuwa na mipango ya kuzungumzia suala hili inaweka utata mkubwa sana na kuthibitisha madai yake, kwamba kuna ufisadi wa makusudi kwenye mifumo ya viza.
Kwa kawaida raia anapokamatwa anatakiwa kupelekwa katika kituo cha polisi cha karibu na kuandikishwa.
Utekaji wa namna hii umefanyika sana wakati wa awamu ya tano, tunaona awamu ya sita pia ikitumia njia hizo hizo kwa watu inaotofautiana nao.
#FreeMadeleka #ChangeTanzania
0 Comment
Leave a Comment