Kuna taarifa za kuaminika kutekwa kwa mwanasheria Peter Madeleka hapo Serena hotel.......!!
Kuna taarifa za kuaminika kutekwa kwa mwanasheria Peter Madeleka hapo Serena hotel, amekekwa na watu wanaoshukiwa kuwa ni askari wasio na uniform na kutoweka nayeNdugu wa Peter Madeleka wameenda Central wanaambiwa hayupo. Wanaelekea Sealander
Madeleka ametekwa na askari waliovaa kiraia na kupotea naye, Haya mambo walifanyika kwa Freeman Mbowe huko Mwanza, Tunaona yanaendelea kwa Watanzania wengine
Serikali ya awamu ya sita inajipambanua kinyuma na matendo kama haya lakini chini kwa chini yanafanyika
Madeleka aliwahi kuwa afisa katika jeshi la polisi, Kosa lake ni kuelezea kuhusu VISA fake ambazo zinatolea Airport , alipanda kuongea na waandishi wa habari kuelezea namn haya mambo yanafanyika, Siku mbili zilizopita alilalamika kwamba Jeshi la Uhamiaji kupitia group lake la WhatssApp walikuwa wakipanga mipango ya kumuua, Leo ametekwa na hapatikani mahali popote pale, hapatikani katika vituo vyote vya polisi ambavyo ndugu zake wameanda kumtafuta,
Kwa kawaida raia anapokamatwa anatakiwa kupelekwa katika kituo cha polisi cha karibu na kuandikishwa.
Utekaji wa namna hii umefanyika sana wakati wa awamu ya tano, tunaona awamu ya sita pia ikitumia njia hizo hizo kwa watu inaotofautiana nao
#FreeMadeleka
0 Comment
Leave a Comment