Hukumu ya kesi ya Freeman Mbowe na wenzake katika shauri namba 3 mwaka 2020 katika mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu Zitto Kabwe, Hashim Rungwe na hayati Maalim Seif walifungua kesi Wakati wa awamu ya tano katika serikali ya hayati Rais Magufuli, utawala ambao ulijitahidi kutumia kila aina ya sheria kuhakikisha wanafifisha maendeleo ya kimekrasia katika nchi yetu.
Wakati wa utawala wa awamu ya tano sheria nyingi zilibadilishwa ili kufifisha maendeleo ya demokrasia katika nchi yetu na moja ya sheria iliyobadilishwa ni sheria ya vyama vya siasa (sheria namba 5 ya mwaka 1992 na mabadiliko yake ) ili kupunguza uhuru wa kidemokrasia, uhuru wa kujumuika kwa watanzania na kufanya siasa. Sheria hiyo ambayo ilitiwa saini na aliyekuwa rais wa taifa hilo , John Pombe Magufuli mwezi Februari mwaka 2019 na kuchapishwa katika gazeti la serikali. Sheria hiyo mpya ilikuja na vipengele ambavyo vilikuwa vinawanyima haki viongozi na wanachama . Baada ya kuona haki haipatikani katika mahakama za Tanzania viongozi hawa wa vyama vya upinzani wakaona haja ya kwenda katika mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) kufungua kesi ili sheria hiyo iangaliwe. kwa sababu pia sheria hiyo ya vyama vya siasa waliona inavunja mojawapo ya mkataba wa Afrika Mashariki ambao unaelezea kwa kirefu nchi zote mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanavyopaswa kuendesha mambo yao ya kidemokrasia katika nchi zao.
Lengo la kesi hiyo kulingana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe ni kwamba sheria hiyo mpya iliwekwa kupitia kubadili na kuongeza baadhi ya vifungu ambavyo vinakiuka lengo la kuanzisha ushirikiano wa jumuiya ya Afrika mashariki.
Katika kesi hiyo Jaji alisoma vipengele kadhaa vya kisheria ambavo vilitumiwa na waleta maombi.
- Vipengele ambavyo vinalalamikiwa kwenye sheria ya vyama vya siasa ni pamoja na kifungu kinachompa Msajili wa vyama vya siasa kuingilia wakati wowote shughuli za chama cha siasa
- Kifungu kinachompa mamlaka msajili awe na mamlaka ya kuingilia mafunzo mbalimbali ya vyama vya siasa.
- Kifungu kinachompa msajili mamlaka ya kuingilia uongozi wa chama cha siasa.
- Kifungu kinachompa msajili kumsimamisha uanachama mwanachama yeyote kushiriki shughuli za kisiasa
Vifungu vyote hivi vinakiuka misingi ya utawala bora, misingi ya kidemokrasia na inakiuka mkataba wa EAC.
Hivo waleta maombi wanaomba mahakama hii itamke kuwa sheria hiyo ni batili na mahakama hii itoe amri kuwapa kila aina ya nafuu ya kisheria.
Mjibu maombi alijibu kuwa kifungu hiki kinalenga kufanya serikali itambue, ijue kila tukio linalofanywa na vyama vya siasa, Na kwamba Mahakama hii inaona kuwa kifungu hiki kinakiuka mkataba wa EAC.
Section 9, Kifungu hiki kinampa msajili mamlaka ya kuchukua orodha ya wanachama/viongozi kutoka kwa vyama vya siasa kwa muda wowote atakaona unafaa. Pia kifungu hiki kinazuia mafunzo ya ukakamavu kwa wanachama wake, mafunzo yoyote au kuunda vikosi kama green guard etc.
Kuhusu kifungu cha tisa cha orodha ya wanachama au viongozi waleta maombi wanasema kifungu hiki kipo shallow mno. Kinatoa haki upande mmoja na kuichukua kwa upande mwingine, jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa chama cha siasa. Kifungu hiki kinaweza kutumiwa vibaya na msajili
Hata hivo mjibu maombi alisema kuwa kifungu hakina shida kabisa na kinatekelezeka bika tatizo lolote Waleta maombi wanasema kuwa ni sheria kusema kuwa maamuzi yafanywe tu na mikutano mikuu ni kuzuia haki hiyo ya kuungana.
Section 15; Waleta maombi wanalalamika Kifungu hiki ambacho kinahusu vyama kuungana kuwa kinakiuka haki ya kukusanyika kwa kuwa kinakosa uhalali hasa kwa kuwa kifungu kinataka muungano uwe tu wakati wa uchaguzi Yaani vyama vinaweza tu kuungana wakati wa uchaguzi mkuu.
Hii ni kinyume cha haki ya kukusanyika Kifungu hiki kinataka uamuzi wa vyama kuungana ufanywe na mikutano mikuu ya vyama vya siasa! Na ufanywe miezi mitatu kabla ya uchaguzi.
Section 29, Kifungu hiki kinasema mtu yeyote atakayekiuka sheria hii atapigwa faini ya milioni moja ambayo haitazidi milioni 10 au kifungo kisichozidi mwaka. Chama cha siasa kikiuka sheria hii kinaweza kupigwa faini hadi milioni 30 au kufutwa.
Msajili ana mamlaka ya kuandika kusudio la kufuta chama cha siasa kitakachokiuka sheria hii na ataandika kusudio hilo kwa wanachama. Hata hivo mjibu maombi anasema kuwa kifungu hiki kimezingatia utawala bora na hakijakiuka mkataba.
Waleta maombi wanasema msajili kuwa na mamlaka ya kuadhibu mwanachama/kiongozi na chama chenyewe ni kuminya haki ya ustawi wa vyama vya siasa Pamoja na kukiuka haki ya kushiriki katika demokrasia kwa wanachama/wananchi. Ni sheria katili inayompa mamlaka ya kiimla Msajili.
Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) ilideclare kuwa sheria ya vyama vya siasa inakiuka vifungu vya mkataba sehemu 6d 72 ya Jumuiya ya Afrika na kuamuru serikali ya Tanzania kurekebisha Sheria ya vyama vya siasa, ili iondoe vifungu vinavyokiuka mkataba ulioianzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), hukumu iliyotolewa kuhusu kesi iliyofunguliwa na wanasiasa wapinzani.
In the East African Court of Justice at Arusha first Instance division.
http://changetanzania.org/wp-content/uploads/2022/03/In-the-East-African-Court-of-Just
0 Comment
Leave a Comment