Nguvu Ya Mitandao Na Nafasi Yake Kudai Katiba Mpya.
#MariaSpaces #WenyeNchiWananchi #KatibaMpya #ChangeTanzania
Katiba ya Tanzania ina mapungufu makubwa kuhusu haki za binadamu ambapo imechangia kwa kiasi kikubwa uvunjifu wa haki za binadamu. Mfano haki ya kutoa maoni ina vikwazo vingi ikiwemo sheria ya makosa ya mitandao. Katiba yetu ina mapungufu makubwa. Tusipozungumza kero zetu kwa mitandao viongozi wanaweza kujua tumeridhika nazo. Nguvu ya wananchi inahitajika kupaza sauti kwenye kila sehemu kuonyesha tumedhamiria kupata mabadiliko. Mitandao ya kijamii ni nyenzo muhimu katika harakati ya #KatibaMpya kwani tumeona ikitumika na mataifa mbalimbali katika kuleta mabadiliko. Watu wa Misri walitumia Twitter katika kupanga maaandamno dhidi ya Mohamed Musri na walifanikiwa kumtoa madarakani. Kupitia kelele za mitandao zimefanya ripoti ya CAG kuairishwa kujadiliwa mwezi Novemba na kujadiliwa baada ya Bunge la kipindi hiki. Tunatakiwa kuunganisha makundi mbalimbali katika mitandao ya kijamii ili kupeana elimu ya #KatibaMpya na harakati za mabadiliko kiujumla. Tutumie mitandao kuchambua maudhui na kuhamasisha wananchi kujua haki zao za msingi, madhara ya katiba ya sasa na manufaa ya #KatibaMpya.
ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi
ENGLISH VERSION
The Constitution of Tanzania has major shortcomings regarding the safeguard of human rights. This has largely contributed to the violation of human rights such as the right to freedom of expression which has many restrictions, including the law of network errors. Our constitution has serious shortcomings such that if we don't talk about our problems online, leaders will assume that we are okay with their existence. The power of the people is needed to raise their voice in every part to show that we are determined to attain change. Social media is an important tool in the movement to demand for a new constitution as we have seen it being used by various nations as a catalyst for change. The people of Egypt used Twitter to organize protests against Mohamed Musri and succeeded in removing him from power. The social media noise raised by citizens concerning the Controller Auditor General (CAG) report has forced the government to move up the discussion of the CAG report after the budget parliament from its prior decision to discuss it in November. We need to unite various groups in social networks to provide education on the shortcomings of the current constitution and the need for a new constitution.
ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi
0 Comment
Leave a Comment