News Details

Bandari, Uporaji Ardhi Na Uhaba Wa Dola - CCM Wanatufukarisha?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Chama cha Mapinduzi imeweka mipango ya kujipatia fedha kwa njia ambazo ni halali lakini fedha haramu. Katika kipindi kifupi tumeshuhudia mlundikano wa tozo lakini pia serikali ikikopa fedha nje kwa kiasi kikubwa sana. Wananchi wamehoji juu ya mafuta kupanda bei kila mwezi na wengi kuhusisha na mpango uliojificha wa serikali kutafuta pesa zaidi kutoka kwa wananchi bila ya kujali hali ya wananchi kwani maisha yamepanda bei na kiwango cha maisha kushuka.  Mambo yanayofanyika nchini kwa jina la uhifadhi ni mambo ya kutisha. Wananchi wa Loliondo na Ngorongoro wanapitia madhira makubwa ya kunyanyaswa katika ardhi yao kwani serikali imewafukuza kwa ulazima kwa sababu za uhifadhi huku tukiona maeneo hayo hayo yakipewa kwa wageni kwa shughuli za uwindaji na ujenzi wa hoteli za kitalii.

 Mifumo yetu ya uongozi inaruhusu watu wa juu kutokuwajibishwa na hii inashuka mpaka kwa watendaji wa chini kwani wanafanya kazi kuwaridhisha walio na nafasi ya juu. Viongozi hawako tayari kukosolewa na wananchi wanaofanya hivyo wanachukuliwa kuwa ni maadui wa taifa. Wananchi inabidi tushikane na tuwe na umoja, tutoke wote kudai katiba mpya na si kuwaachia wanaharakati tuu. Hii nchi ni ya yetu na tuna mamlaka ya kukosoa viongozi endapo wata

#ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi 

 

ENGLISH VERSION

Chama Cha Mapinduzi has made plans to get illegal money from citizens in ways that are legal. In a short period of time, we have witnessed the accumulation of taxes imposed on the people but also the government external borrowing in a very large amount. Citizens have questioned the increase in oil price every other month and many have associated it with a hidden plan of the government to loot more money from the citizens with little regard to their condition as the cost of living has increased causing a fall in the standard of living. 

The things that are happening in the country in the name of conservation are terrible things. The people of Loliondo and Ngorongoro are going through great consequences of being forcefully evacuated from their ancestral land as the government has driven them out of necessity for reasons of conservation while we see the same areas being given to foreigners for hunting activities and the construction of tourist hotels. Our leadership systems allow the top people to not be held accountable and this trickles down to the bottom performers as they work to please those in higher positions. Leaders are not ready to be criticized and citizens who do so are considered enemies of the nation. Citizens, we have to stick together and be united, we all come out to demand a new constitution and not just leave it to the activists. This country is ours and we have the authority to criticize the leaders if they want

#ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi

0 Comment

Leave a Comment