News Details

Harakati Na Mitandao, Mbinu Za Kulinda Harakati Karne Ya 21

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Dunia kwa sasa inatambua nguvu ya mitandao, kuna mabadiliko yamefanywa duniani kutokana na nguvu ya mitandao. Kwa sasa mikutano mingi sana inafanyika kidigitali na kuwakusanya watu zaidi. Harakati nyingi za mabadiliko hasa ya kimfumo katika utawala hutegemea zaidi mitandao ya kijamii hasa katika karne ya 21 kunatokana kukua kwa  utandawazi. Serikali kwa kutambua hili inafanya jitihada kubwa sana kuzima mitandao ya kijamii kutokana na nguvu ya umma kutumia zaidi mitandao kuwasiliana kuhusu masuala ya wananchi. Katika kubana na kuzuia matumizi ya mitandao ya kijamii Serikali imekua ikipandisha bei ya mabando na kuleta sheria kandamizi zinazozuia uhuru wa wananchi katika kutoa maoi au habari kwenye mitandao jambo ambalo linaenda kinyume na haki za binnadamu pamoja na katiba. Wananchi wana wajibu wa kulinda nafasi yao kama wenye nchi.

 Wananchi waelimishane wenyewe kwa wenyewe juu ya kutumia mitandao ya kijamii kukuza nguvu ya umma katika kuleta mabadiliko hasa katika karne hii ya 21. Harakati ni ishara ya uhai, wananchi wanazungumza mapungufu mbalimbali ya serikali katika utendaji wake na kutetea maslahi yao kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla. Wajibu wa serikali ni kushughulikia changamoto na maoni ya wanaharakati ambao mara zote wamekuwa ni wawakilishi wa wananchi wanyonge wasioweza kujisemea changamoto zao, lakini badala yake imekua ikiwapiga vita. Wananchi wanahitaji kuunganna katika kutumia mitandao kwa sababu inaweza kuwa chachu ya kuleta mabadiliko katika Taifa letu. Tunatakiwa kuimarika kutumia mtandao kwa kuwa ni sauti inayofika haraka na utawala huona malalamiko ya wananchi hasa kwa kipindi hiki ambacho mitandao ya kijamii imeshika hatamu. 

#ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi 

 

ENGLISH VERSION 

The world is now realizing the power of social networks, changes have been made in the world due to the power of socialnetworks. Currently, many meetings are held digitally and these platforms gather a lot of people. Many movements for systemic changes in governance depend more on social networks, especially in the 21st century due to the growth of globalization. Realizing this, the government is making a huge effort to shut down social networks as they provide avenues to the public to communicate on the issues and challenges they face.
In restricting and preventing the use of social networks, the Government has been increasing the price of internet bundles and introducing oppressive laws that prevent citizens from freely giving their opinions or information on social networks, which goes against human rights as well as the constitution. Citizens have a responsibility to protect their position as the true owners of the country. Citizens should educate each other about using social networks to promote the power of the public in bringing about change especially in this 21st century. The government's responsibility is to deal with the challenges and opinions raised by activists who have always been representatives of citizens who cannot speak for themselves about their challenges, but instead it has continually fought against them. Citizens need to unite in using social networks as it can be a catalyst for bringing about change in our nation as the platform amplifies our voice to reach the respective authorities quickly, especially in this period when social networks have taken over.

#ChangeTanzania   #WenyeNchiWananchi

0 Comment

Leave a Comment