News Details

Kero Za Muungano Zimeongezeka au Zimepungua?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Muungano ulikuwa ni makubaliano ya kati ya waasisi wawili na si makubaliano ya wananchi wa pande mbili. Tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, maadiliko megi yametokea hivyo kupelekea changamoto malimbali za muungano. Kwa sasa kuna wananchi wanaotaka muungano wa Tanganyika na Zanzibar uendelee kuwepo lakini kuwe na serikali tatu.  Baadhi ya wananchi wanasema wazanzibari wananufaika zaidi na muungano kuliko watanganyika. Hii ni kutokana na kwamba wazanzibari wanaruhusiwa kumiliki ardhi, kuajiriwa na kujihusisha na siasa za Tanzania bara lakini watanganyika hawaruhusiwi kufanya hivi vyote wakiwa Zanzibar. Kipindi tunapata muungano kulikiwa na idadi ya watu million 6 kwa Tanganyika na laki tatu kwa Zanzibar, kwa sasa kuna mabadiliko makubwa, hivyo tunahitaji kuzingatia mabadiliko hayo na kusuka sheria mpya hasa tukizingatia muungano. Watanzania wanahitaji muungano unaobeba hali halisi ya wananchi wanavyotaka na sio kikundi kidogo cha watu. Ili kupunguza kero za muungano serikali inabidi ikae kwa upya na kupitia kipengele vyote vya maeneo ya muungano ili kuleta usawa kati ya Tanganyika na Zanzibar. Hii itawezeshwa tukiwa na katiba bora ambayo kila mmoja ataona fahari kuwa sehemu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. 

#ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi 

 

ENGLISH VERSION 

The union was an agreement between the two founders and not an agreement between the citizens of the territories of Tanganyika and Zanzibar. Since the union of Tanganyika and Zanzibar in 1964, many conflicts have occurred, leading to various challenges to the union. At the moment there are people who want the union of Tanganyika and Zanzibar to continue to exist but there should be three governments. Some citizens say that people from Zanzibar benefit more from the union than those from Tanzania mainland. This is due to the fact that the people of Zanzibar are allowed to own land, be employed and get involved in the politics of Tanzania mainland, but the people from the mainland are not allowed to do all this while in Zanzibar.

 While we are uniting the two territories Tanganyika had a population six million people with that in Zanzibar being three hundred thousand, currently so many big changes have taken place hence, we need to consider the changes and weave new laws with special consideration for the union. Tanzanians need a union that reflects the current needs of the people and not a small group of people. In order to reduce the union problems, the government has to sit anew and go through all aspects of the union so as to bring balance between Tanganyika and Zanzibar. This will be facilitated if we have a better constitution in which everyone will be proud to be part of the union of Tanganyika and Zanzibar.

#ChangeTanzania  #WenyeNchiWananchi 

0 Comment

Leave a Comment