News Details

Tunaimarishaje Nguvu Ya Umma Inayowezeshwa Na Mitandao?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Hatuwezi kupuuzia nguvu ya mtandao kuwa kuwa siku hizi inatumika na watu wengi kufikisha habari muhimu. Mitandao ya kijamii inasidia kutuleta pamoja ili kukamilisha malengo yetu hasa katika kupata mabadiliko na haki. Kupitia mitandao tunaweza kuimarisha nguvu ya umma kwa kuweza kuhoji serikali. Wananchi wasipozungumza kero zao kwenye mitandao viongozi wanaweza kujua wameridhika nazo. Wananchi inabidi watumie mitandao ya jamii kupaza sauti kila sehemu kuonyesha dhamiria ya kupata mabadiliko. Wananchi wanatakiwa watumie mitandao kuchambua maudhui na kuhamasisha wananchi wengine kujua haki zao za msingi, kuelimishana kupitia mitandao madhara ya katiba ya sasa na manufaa ya #KatibaMpya.

 Hii itarahisiaha harakati za kudai #KatibaMpya. Nguvu ya umma itaimarishwa pia endapo makundi mbalimbali katika mitandao ya kijamii yakiungana ili kupeana elimu ya #KatibaMpya na mbinu za harakati za mabadiliko kiujumla. Kupitia kelele za mitandao zimefanya ripoti ya CAG kuhairishwa kujadiliwa mwezi Novemba na kujadiliwa baada ya Bunge la kipindi hiki, huu ni mfano kuwa hata ipo siku tutapata #KatibaMpya . Tunatakiwa kujiunga sisi Watanzania katika kutumia mitandao kwa sababu inaweza kuwa chachu ya kuleta mabadiliko katika Taifa letu. Tunatakiwa kuimarika kutumia mtandao kwa kuwa ni sauti inayofika haraka na utawala huona malalamiko ya wananchi hasa kwa kipindi hiki ambacho mitandao ya kijamii imeshika hatamu. 

#ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi 

 

ENGLISH VERSION 

We cannot ignore the power of social media as it is used by many people today to convey important information. Social media helps bring us together to accomplish our goals, especially in achieving societal change and justice. Through social networks we can strengthen the power of the public by being able to question the government. When citizens do not talk about their problems on the internet, government leaders may be reluctant to solve these problems thinking that the citizens are comfortable with their existence. Citizens have to use social media platforms to raise their voice everywhere to show the determination to achieve change. Citizens should use social platforms to analyze and share useful content that will encourage other citizens to know their basic rights, educate each other on the effects of the current constitution and the benefits the nation will derive from a new constitution. 

This will easily facilitate the people’s movement to demand for a new constitution. The power of the public will also be strengthened if various groups in social networks unite to provide education on the need for a new constitution and the peaceful methods that can be used in the movement for change. Through citizen’s noise on social media platforms concerning the CAG report, the government postponed it from being discussed in November but rather in the next parliamentary sessions. This stands to show that through raising citizens' voices, even obtaining a new constitution will be possible. We Tanzanians need to join our voices in social platforms as it can be used as a catalyst to bring about change in our nation. We need to strengthen the use of social media in advancing our needs to the government as the platforms make it easy for our voices to be heard especially in this period where the use of social media has taken over.

#ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi

0 Comment

Leave a Comment