Katiba Mpya Ya Warioba Bila Katiba Ya Tanganyika Haiwezekani - Tufanyeje?
#MariaSpaces #WenyeNchiWananchi #KatibaMpya #ChangeTanzania
Wananchi wa Tanzania wamekua wakidai #KatibaMpya kwa muda mrefu sasa lakini Rasimu ya Warioba ikifanikiwa kuwa #KatibaMpya haitaweza kutimia bila ya kuwa na katiba ya Tanganyika. Kuna Serikali ya Tanganyika, ya Zanzibar na ya Muungano lakini Rasimu ya Warioba imeandikwa ikitoa muongozo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sehemu za muungano ni maeneo 7 tuu hivyo kuacha maeneo mengine bila kuguswa.
Kuna migogoro mingi ya muungano baina ya wananchi kama vile, Mtanganyika hana haki ya kushiriki siasa wala kumiliki ardhi Zanzibar lakini Wazanzibari wanapata haki hiyo Tanganyika. Ili Changamoto za Muungano ziweze kutatuliwa inabidi kuwe na Katiba ya Tanganyika na maboresho yafanyike kwenye katiba ya Zanzibar ili iweze kuendana na Katiba ya Muungano. Mchakato wa kutengeneza katiba ya Tanganyika utarahisisha upatikanaji wa katiba ya Muungano kwani ni jambo la muhimu kufanyika ili tuwe na mazingira yanayoruhusu nchi washirika kuwa huru na kunufaika na Muungano.
#ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi
ENGLISH VERSION
The Tanzania people have been demanding a new constitution for a long time now, but if the Warioba Draft succeeds in becoming a new constitution, it will not be able to come true without Tanganyika having its own constitution in place. There is a Tanganyika, Zanzibar and Union Government but the Warioba Draft has been written to guidance to the Union government of Tanzania and areas under which the Zanzibar and Tanganyika cooperate in were as there are only seven areas leaving other areas untouched, something that has led to a number of challenges to that threaten the existence of the union.
Such challenges include; the inability of Tanzanians from the mainland to participate in politics or own land in Zanzibar, but Tanzanians from the isles of Zanzibar get to have the right to do so in Tanganyika. In order for union challenges to be resolved, there must be a constitution of Tanganyika in place and improvements should be made to the constitution of Zanzibar so that it can be compatible with the Union Constitution. The process of making the Tanganyika constitution will facilitate a swift acquisition of the Union Constitution. This is an important thing to be done so that we can have an environment that allows both partner countries to be independent and benefit from the Union.
#ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi
0 Comment
Leave a Comment