News Details

Tutafanikisha Vipi Harakati Ya Kupinga Kodi / Tozo Holela?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Kwa kipindi cha hivi karibuni Serikali yetu imeongeza na kuleta kodi mpya nyingi ambazo zimekua mzigo kwa wananchi hasa wa kipato cha chini. Athari ya mlundikano wa kodi zinazotozwa kwa wafanyabiashara imeonekana kuwa kero kwa wafanyaboashra ambao wameamua kuitisha mgomo wa kufungua maduka yao kwa sababu ya matatizo ya kodi lukuki zinzopelekea mazingira magumu ya utendaji wa kazi yao na kuomba kukutana na Rais ili kuwasilisha matatizo yao.  Wananchi wengine wameishutumu Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA kwa kutengeneza mazingira ya rushwa kwa wafanyabiashara. Hii imechangiwa na ukosefu wa kiwango elekezi cha ushuru wakati wa utoaji wa bidhaa za wafanyabiashara kutoka bandarini, kwa bidhaa zinazoingizwa kutoka nchi za nje na kuuzwa kwenye soko hilo.

Wananchi wamehoji kuwa wawekezaji kutoka nje ya nchi ndio wanaonufaika na biashara lakini si wananchi kwani Serikali hutoa kipindi cha neema cha miaka mitano kwa wawekezaji kutoka nje wanaokuja kufanya biashara nchini lakini hutoza kodi nyingi kwa wananchi wake. Serikali yetu haiangalii njia za kukuza biashara badala yake inatafuta njia mbalimbali za kunyonya mapato ya wananchi wake. Tunahitaji katiba mpya ambayo viongozi watachagulia na kuteuliwa kwa muujibu wa sheria na si kwa matakwa ya rais ili kupata viongozi watakao tumikia wananchi na maslahi yao. 

#ChangeTanzania   #WenyeNchiWananchi 

ENGLISH VERSION

In the recent period, our Government has increased and introduced many new taxes that have become a burden for citizens, especially those with low incomes. The effect of the accumulation of taxes charged to traders has been seen as a nuisance to the traders from Kariakoo market who have decided to call a strike and demand a meeting with the president inorder to address this problem which makes it difficult for business to perform well. Some citizens have gone further to accuse the Tanzania Revenue Authority, TRA for creating an environment of corruption for businessmen. This is due to the absence of a recognised official channel that guides tax payment in moving imported goods from the port to be sold in the market.

Citizens have argued that investors from abroad are the ones who benefit from doing business in the country but not the citizens. This is because the Government provides a 5 year grace period from paying taxes to investors from abroad who come to do business in the country but charge a number of burdensome taxes to its citizens. Our government is not looking at ways to promote business, but instead it is looking for various ways in which it can absorb the little income made by its citizens. We need a new constitution in which leaders will chosen and be appointed according to the law and not according to the wishes of the president in order to put in place leaders who will serve the people and their interests.

#ChangeTanzania   #WenyeNchiWananchi

0 Comment

Leave a Comment