News Details

Kwa Nini Uporaji Ardhi Umeshika Sana Kasi Awamu Hii?

#MariaSpaces  #WenyeNchiWananchi  #KatibaMpya #ChangeTanzania 

Uporaji wa ardhi umeshika kasi tangu 2021. Serikali kutenga maeneo tengefu ni chanzo kikubwa cha unyanganyi wa ardhi kwa wananchi. Hasara ya serikali kutangaza maeneo ya wananchi kuwa hifadhi imefuta haki za wananchi wa maeneo hayo kumiliki ardhi. Tumeona mfano wa hivi karibuni wa wananchi wa Ngorongoro waliolazimika kuhama makazi yao ya muda mrefu kupisha uhifadhi. Maeneo ya hifadhi kuongeza mipaka ya hifadhi pia kumechangia kwa kiasi kikubwa katika uporaji wa ardhi za wananchi.


Mipaka ya magharibi mwa Serengeti umekua mfano katika hili kwani mipaka ya sasa ni kilometa 50 mbele ukilinganisha na ilivyo kuwa mwaka 1959. Matukio haya ya uporaji ardhi ya wananchi na seikali imeacha wananchi wakiuliza kama ni sawa kwa serikali kutenga ardhi kwa manufaa ya wachache na kudhuru maelfu ya watanzania. Kwani kama ilivyoonekana Ngorongoro Serikali imesitisha huduma za muhimu za jamii na huduma za afya ili kulazimisha wananchi waliopo waondoke ili kupisha maeneo yao kufanyika mapori tengefu na hifadhi. 

Serikali katika juhudi zake za kukuza miji imepelekea baadhi ya watanzania kuporwa maeneo yao ili kupisha ujenzi wa miji ya kisasa. Inakadiriwa wakazi zaidi ya 250,000 wa Mabwepande watakabiliwa na tishio la kunyanganywa maeneo yao kwa ajili ya kupisha ujenzi wa satellite city kama ya Kigamboni. Katika haya yote, Serikali imeonekana ikipora ardhi za wananchi kwa ajili ya maslahi ya wachache.  

#ChangeTanzania  

#WenyeNchiWananchi 

ENGLISH VERSION

Land grabbing has picked up pace since 2021. The government's allocation of residential areas as conservation areas has been a major source of land grabbing for citizens. The cons of the government declaring the people's residential areas as a reserve has canceled the rights of citizens to own land. We have seen a recent example of the people of Ngorongoro who were forced to move from their long-term ancestral lands to give way for conservation. Another reason that leads to land grabbing is the increase in boundaries of conservation areas from their initial boundary plans.
This has also contributed significantly to the looting of people's lands, a good example is seen in the western borders of the Serengeti where as today they are 50 kilometers ahead from their initial outlay in 1959. These incidents of looting of the people's land by the government have many citizens questioning if it is right for the government to allocate land for the benefit of the few and harm thousands of Tanzanians as was seen in the Ngorongoro case, the Government has suspended important community services and health services to force the existing citizens to leave in order to turn their areas into isolated forests and reserves.

The government in its efforts to develop cities has led some Tanzanians to be robbed of their lands in order to allow the construction of modern cities. It is estimated that more than 250,000 residents of Mabwepande will face the threat of having their areas taken away for the construction of a satellite city like Kigamboni. In all these, the Government has been seen looting the lands of the people for the interests of the few.

0 Comment

Leave a Comment