Tutapataje Mshikamano Wa Makundi Katika Jamiii Kudai Katiba Mpya?
Mshikamano hauwezi kupatikana bila ya kuwa na mabadiliko ya fikra/mawazo kwa watanzania kuwa mabadiliko yapo mikononi mwao na kila mwananchi ana sehemu ya kufanya ili mabadiliko tunayoyategemea na kutarajia yapatikane. Vijana mtaani wamekuwa mstari wa mbele kushabikia mambo ya michezo na burudani na hawana uelewa wa kina na mambo yanayoendelea nchini kisiasa Elimu ya uraia ikitolewa kwa vijana hawa itaongeza nguvu ya kudai katiba mpya. lakini pia kwenye masoko watu wapewe elimu ya uraia. Wananchi pia wamekubaliana kufanya harakati mtaani ili kuwapa watu elimu ya katiba mpya na majukwaa ya kuwawezesha kujifunza zaidi juu ya nchi yao kama kusikiliza space.
Wananchi pia wamepaza sauti za makanisa na misikiti juu ya nafasi yao katika kudai katiba mpya na kwamba uhusika wao ni wa muhimu katika kufanikisha jambo hili lenye manufaa ya kudumu kwa watanzania wote. Katika kuwezesha mshikamano katika madai ya katiba, wananchi pia wamehamasishana kuanza kuhamasisha na kuelimisha mtu mmoja moja kwenye jamii zao kuanzia katika ngazi ya familia na majirani.
#ChangeTanzania #MariaSpaces #WenyeNchiWananchi
ENGLISH VERSION
Solidarity cannot be achieved without a change in the mindset of Tanzanians that change is in their hands and that every citizen has a part to play so that the changes envisioned can be achieved. Young people have been at the forefront in entertaining sports and gossip with little or no understanding of what is going on in the country politically. If citizenship education is given to these young people, it will increase the power to demand a new constitution. Citizenship education should also be given in the market places to ensure that awareness is made to a greater audience.
Citizens have agreed to carry out a movement in the street to impact people with knowledge on the need and importance of attaining a new constitution and expose them to platforms (Maria Space twitter discussions) that will enable them to learn more about what is taking place in their country. Citizens have also called upon religious leaders on the important role they can play towards the demands for a new constitution which has lasting benefit to all Tanzanians. In facilitating solidarity in constitutional claims, citizens have also encouraged each other to start mobilizing and educating people in their communities starting at the family and level.
#ChangeTanzania #MariaSpaces #WenyeNchiWananchi
0 Comment
Leave a Comment