Report Details

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Kuhusu Ripoti Za Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali Kwa Mwaka Wa Fedha Ulioishia Tarehe 30 Juni, 2018

Katika ukaguzi wangu, nilifanya tathmini ya utekelezaji wa mapendekezo ya kiukaguzi yaliyotolewa miaka iliyopita na kubaini kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuyafanyia kazi. 

Tathmini ya utekelezaji wa mapendekezo hayo inaonesha kuwa kati ya mapendekezo 350 yaliyotolewa miaka iliyopita, mapendekezo 80 sawa na asilimia 22.9 yametekelezwa kikamilifu. Mapendekezo 124 sawa na asilimia 35.4, utekelezaji wake unaendelea. Hata hivyo, mapendekezo 72 sawa na asilimia 20.6 utekelezaji wake haujaanza; na mapendekezo 74 sawa na asilimia 21.1 yamepitwa na wakati

Katika Ukaguzi wa Hesabu nilioufanya kwa Serikali Kuu na Taasisi zake, Mamlaka za Serikali za Mitaa, na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha 2017/18, nimetoa jumla ya Hati 548 za Ukaguzi. Kati ya hizo, Hati zinazoridhisha ni 531, sawa na asilimia 97; Hati zenye shaka ni 15, sawa na asilimia 2.6; Hati 1 isiyoridhisha, ambayo ni sawa na asilimia 0.2; na Hati mbaya 1, sawa na asilimia 0.2.


Posted on : 13 April, 2019 DOWNLOAD REPORT