Ripoti Ya Mwaka Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali Kuhusu Ukaguzi Wa Mashirika Ya Umma Kwa Mwaka Wa Fedha 2016/2017
Ripoti ya mwaka ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kuhusu ukaguzi wa mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha 2016/2019. Kwa mujibu wa Ibara ya 143 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na mabadiliko na kama ilivyoainishwa katika Sehemu ya 11(4) ya Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya mwaka 2008, mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali aliwasilisha ripoti ya mwaka ya ukaguzi wa mashirika na taasisi nyingine za umma kwa mwaka wa fedha 2016/17, bungeni kulingana na matakwa ya sheria.