Ripoti Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali Kuhusu Ukaguzi Wa Miradi Ya Maendeleo Kwa Mwaka Ulioishia Tarehe 30 Juni, 2017
Sehemu hii ya ripoti inatoa maelezo ya jumla ya matokeo ya ukaguzi wa taarifa za hesabu yanayotakiwa kuzingatiwa kwa umakini na Serikali, Bunge, Maafisa Masuuli na Wadau wengine wa miradi ya maendeleo.
Taarifa hii inajumuisha muhtasari wa mambo muhimu yaliyotokana na ukaguzi ambapo taarifa zake kwa ujumla zimeelezwa katika barua ya mapungufu na katika taarifa ya ukaguzi inapelekwa kwa watekelezaji wa miradi. Katika ripoti hii tumewasilisha mambo ambayo tumeona ni ya muhimu kuletwa kwa Serikali, wasimamizi wa taasisi pamoja na Umma.
Aidha, nimegundua mapungufu katika masuala ya usimamizi wa fedha na bajeti, mifumo ya ndani, na usimamizi wa kanuni na sheria. Mapungufu haya yanahitaji kufanyiwa kazi na watekeleza miradi ili kuboresha utendaji katika siku zijazo.