Ripoti Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali Kuhusu Ripoti Za Ukaguzi Wa Ufanisi
Ukaguzi wa Ufanisi unalenga kuboresha uwajibikaji na ufanisi wa taasisi za umma. Pia, unatoa tathmini mahsusi ya namna taasisi ziliokaguliwa zilivyotumia raslimali katika kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia uwekevu, tija, na ufanisi. Kifungu Namba 28 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma Namba 11 ya Mwaka 2008 kinampa mamlaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya Ukaguzi wa Ufanisi.
Ripoti hii ya jumla inaainisha mapungufu yaliyobainika, hitimisho, na mapendekezo ya ripoti saba za ukaguzi wa ufanisi katika sekta ya kilimo uliofanyika kati ya mwaka 2015 na 2019 kuhusu utoaji wa huduma kwa wakulima; milipuko ya magonjwa na visumbufu vya mimea; viuwatilifu kwenye shughuli za kilimo; utoaji msaada na huduma kwa wajasiriamali wadogo na wa kati; upatikanaji na ufikiaji wa pembejeo za kilimo bora kwa wakulima; usimamizi wa shughuli za ujenzi wa miradi ya umwagiliaji; na utoaji wa huduma za ugani, ambayo inajumuisha taarifa ya ufuatiliaji.
Mtazamo huu maalumu kwenye eneo la kilimo umetolewa ili kutathmini jinsi serikali inavyosimamia maendeleo ya kilimo katika kuhakikisha ufanisi, ushindani, na faida ya sekta ya kilimo katika kuchangia kuboresha maisha ya Watanzania kufikia ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
Ripoti hii inabainisha masuala muhimu yaliyobainika katika kaguzi za ufanisi zilizofanywa dhidi ya kile kilichotarajiwa katika upande wa utoaji wa huduma.
Kwa ujumla Ripoti hii ina lengo la kuwasaidia wabunge, serikali, vyombo vya habari, umma, na wadau wengine kuweza kufanya maamuzi yenye kuongeza uwekevu, tija, na ufanisi katika utendaji wa serikali katika sekta ya kilimo. Aidha, Ripoti hii ya majumuisho hailengi kuwa mbadala wa ripoti saba zilizowasilishwa katika miaka tajwa ya kifedha. Hivyo, msomaji anashauriwa kusoma ripoti za ukaguzi husika ili kuweza kupata undani wa kilichokaguliwa.
Ripoti hii inatoa ufafanuzi wa ripoti mojamoja za ukaguzi wa ufanisi kuhusu kiwango ambacho taasisi za serikali zinasimamia maendeleo ya sekta ya kilimo na kuhakikisha kuna ufanisi katika utekelezaji wa hatua zake katika maendeleo ya sekta ya kilimo. Yafuatayo ni matokeo makuu ya ukaguzi kutoka kwenye kaguzi zilizofanywa