Report Details

Ripoti Kuu Ya Mwaka Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali Juu Ya Taarifa Za Fedha Za Serikali Kuu Kwa Mwaka Ulioishia Tarehe 30 Juni, 2017

Sehemu hii ya taarifa ya ukaguzi wa jumla wa Serikali kuu inatoa muhtasari mfupi wa matokeo makubwa, hitimisho na mapendekezo ya Ukaguzi. Ripoti hii imejumuisha ukaguzi wa Mafungu 65 ya Wizara na Idara ya Serikali, Wakala za Serikali 35, Mifuko Maalum ya Fedha 17, Taasisi Nyingine za Serikali 38, vyama vya siasa10; Sekretarieti za Mikoa 26, Balozi 39, Bodi za Maji ya Bonde 13. Pia taarifa hii inajumuisha ukaguzi wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania, Akaunti ya Jumla, ukaguzi wa awali wa Taarifa za Pensheni na ukaguzi maalum.

Kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Kati ya taasisi 241 zilizokaguliwa Taasisi 237 zimekaguliwa na kupewa hati ya Ukaguzi wa hesabu waliozo andaa. Balozi za Tanzania 4 hazikupata hati za Ukaguzi kwa sababu ndio kwanza zimeanzishwa. Mlinganisho wa hati za ukaguzi kwa miaka mitatu iliyopita ni kama ionekanavyo hapo chini 


Posted on : 21 March, 2019 DOWNLOAD REPORT