Report Details

Ripoti Kuu Ya Mwaka Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali Juu Ya Taarifa Za Fedha Za Mamlaka Ya Serikali Za Mitaa Kwa Mwaka Wa Fedha 2017/18

Nimefanya ukaguzi wa Taarifa za Fedha kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa 185, na nimetoa hati mbalimbali kwa kaguzi zilizofanyika.

Nimefanya tathmini ya hati za ukaguzi zilizotolewa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa muda wa miaka minne na jinsi gani mwenendo wa hati za ukaguzi unaathiri mwelekeo wa kimkakati na maendeleo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa. Ikilinganishwa na ukaguzi wa mwaka ulipita, Mamlaka za Serikali za Mitaa zenye hati zinazoridhisha zimeongezeka kutoka 166 hadi 176, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4. Pia, Mamlaka za Serikali za Mitaa zenye hati zenye shaka zimepungua kutoka 16 hadi 7, sawa na asilimia 5.

Aidha, hati zisizoridhisha zimepungua kutoka 3(%) hadi 1(%), hii inaashiria maboresho katika utayarishaji wa taarifa za fedha; kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2013/2014, Mamlaka ya Serikali za Mitaa moja ndio imepata hati mbaya (Disclaimer of Opinion).

Hatua stahiki zinahitajika kuchukuliwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ambayo katika miaka minne mfululizo, imepata hati isiyoridhisha. Tahadhari hiyo hiyo inahitajika katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ambayo imepata Hati yenye shaka kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.


Posted on : 13 April, 2019 DOWNLOAD REPORT