Report Details

Ripoti Kuu Ya Mwaka Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali Juu Ya Taarifa Za Fedha Za Mamlaka Ya Serikali Za Mitaa Kwa Mwaka Wa Fedha 2016/2017

Ripoti hii imejumuisha matokeo muhimu ya Ukaguzi wa Mamlaka ya Serikali za mitaa, hasa kwenye tathmini na uchunguzi wa taarifa za fedha pamoja na kumbukumbu zake, udhibiti wa mifumo ya ndani taratibu, pamoja na michakato ya manunuzi na kufuata sheria na kanuni. Pia, inajumuisha matokeo ya Ukaguzi Maalumu uliofanywa na utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi ya miaka ya nyuma na maelekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa mwaka 2016/2017. 

 Kufuatia Ukaguzi uliofanyika, maoni ya ukaguzi yametolewa kwa Mamlaka za serikali za mitaa zipatazo 185 ambazo zilikaguliwa, na nimeweka wazi katika maoni hayo kama taarifa za kifedha zinaonesha mtazamo wa kweli na wa haki kwa mujibu wa viwango vilivyopitishwa vya kimataifa vya mfumo wa uaandaaji taarifa wa hesabu katika sekta ya umma. 

 Ukaguzi ulifanyika kulingana na Viwango vya Kimataifa kwa Taasisi Kuu za Ukaguzi (ISSAIs) iliyotolewa na Viwango Mahususi kwa Ukaguzi wa Taasisi za Umma vinavyotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Wahasibu (IFAC) ambazo ni muhimu kwa ajili ya ukaguzi wa sekta za umma. Ofisi yangu


Posted on : 21 March, 2019 DOWNLOAD REPORT