Malalamiko Yaliyokithiri Kuhusu Huduma Ya Mabasi Ya Mwendokasi - UDART
ChangeTanzania tumekuwa tukipokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wanachama wetu na wananchi mbalimbali, kuhusu huduma wanazopata kutoka katika taasisi za serikali na binafsi. Tumekuwa tukiwasilisha hizo taarifa kwa wahusika ili hatua au maboresho yafanyike. Kwa muda mrefu tumekuwa tukipokea taarifa za malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu huduma wanazopata katika matumizi ya mabasi ya mwendokasi (UDART).
Nyingi ya changamoto hizi zimekuwa zinajirudia mara kwa mara katika usafiri huu. ChangeTanzania tumekusanya maoni ya wananchi wanaotumia usafiri huu ili kujua matatizo sugu kwa misingi ya kuwasilisha kwenye mamlaka husika ili zipate fursa ya kuzishughulikia changamoto hizo......