Report Details

Kuwasilisha Ripoti Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali Kuhusu Ripoti Kumi Za Ukaguzi Wa Ufanisi Ya Mwaka 31 Machi, 2018

Ukaguzi wa Ufanisi unalenga kuboresha muundo wa uwajibikaji na utendaji wa taasisi za serikali. Pia, unatoa tathmini huru ya namna ambavyo taasisi hizo zinatumia rasilimali katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia uwekevu, tija, na ufanisi. Kifungu cha 28 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, namba 11 ya mwaka 2008 inampa mamlaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya kufanya ukaguzi wa ufanisi kwenye sekta ya umma. 

Taarifa hii ya jumla ya ukaguzi inaelezea mapungufu ya jumla yaliyobainika, hitimisho, pamoja na mapendekezo katika Ripoti kumi (10) za Ukaguzi wa Ufanisi uliofanyika mwaka 2014 na 2017 unaohusu usimamizi wa samani za barabarani; ukaguzi wa vyombo usafiri wa majini; ukaguzi magari na udhibiti wa mwendokasi; ukaguzi wa chakula na ufuatiliaji wa mitambo ya usindikaji na maeneo ya kuingizia chakula nchini; Udhibiti katika uzalishaji uchakataji wa nyama; Usimamizi wa usalama dhidi ya majanga ya moto katika majengo ya umma; tathmini za athari za mazingira katika maendeleo ya miradi; usimamizi wa mipango-miji; usimamizi wa mifumo ya udhibiti wa mazingira katika sekta ya madini; na kaguzi za ufuatiliaji. 

Kwa ujumla, ripoti hii inalenga kuwasaidia wabunge, serikali, vyombo vya habari, umma, pamoja na wadau kufanya maamuzi sahihi ili kutekeleza pendekezo la kubana matumizi, na kuongeza tija na ufanisi kwenye kulinda usalama na afya kwa watumiaji mbalimbali wa huduma. Hata hivyo, ripoti hii haijalenga kuwa mbadala wa ripoti zingine kumi za ukaguzi zilizotajwa ambazo zilifanyika mwaka wa fedha uliopita. Hivyo basi, msomaji wa ripoti hii anashauriwa kuzingatia zaidi ripoti husika.


Posted on : 21 March, 2019 DOWNLOAD REPORT