Utawala Bora Na Rushwa Ya Madaraka.

Pamoja na changamoto nyingi  tulizonazo Tanzania, kukosa huduma muhimu  maji,  umeme, huduma mbovu za afya, miundombinu isiyozingatia viwango vya usalama, tozo, na mengine mengi katika nchi yetu, Lakini tuna tatizo lingine kubwa ambalo  tumesababishiwa na watalawa kwa manufaa yao wenyewe  kukosa utawala bora ambao chanzo chake kikubwa ni vyeo vya kupeana kama shukurani, kuna wengine wanasema ni RUSHWA ( fursa, fedha na madaraka)  iliyokithiri na inayoendekezwa na watawala.

Dhana ya Utawala Bora ina nguzo kuu sita

  • Katiba ya kidemokrasia;  
  • Ulinzi, ukuzaji na uzingatiaji wa haki za binadamu;
  • Mgawanyo wa Madaraka;  
  • Uhuru wa Mahakama;  
  • Uhuru wa habari na 
  • Uhuru wa vyombo vya habari.

Kati ya vitu ambavyo utawala wa Tanzania unakosa ni utendaji wa ukamilifu wa vitu vyote tajwa hapo juu hasa kiutendaji zaidi, kwa kuwa serikali ya CCM imekuwa ikifanya na kuamua mambo yake kibabe pengine bila hata ridhaa ya wananchi. Lakini pia serikali ya CCM imekuwa ikichezea chaguzi, kumekuwa na matukio ya fujo na wizi wa kura wa waziwazi wakati wa chaguzi, wapinzani wamekuwa wakiondolewa kwenye mchakato kwa nji za fitina, lakini wagombea wote wa chama cha mapinduzi wamekuwa wakipitishwa na Tume ya Uchaguzi kugombea bila makosa kwenye fomu, lakini pia tumeona baada ya wagombea wa CCM wakipewa majimbo na TUME ya UCHAGUZI kwa hoja ya kupita bila kupingwa !!! lakini hii yote inatokana na mikakati ya Tume ya Uchaguzi kudondosha kimkakati wagombea kutoka vyama vya upinzani 

Katiba yetu ya Tanzania ya 1977 imempa madaraka makubwa Rais ikiwemo nguvu kubwa na nafasi nyingi za teuzi katika nafasi mbalimbali za uongozi kama mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu na wengine wengi. Hii ni hatari kwa kuwa mamlaka yanatoka kwa Rias na sio wananchi ambao wataongozwa na viongozi hao, matokeo yake viongozi hao watakuwa wanafanya kumfurahisha Rais ili wapate teuzi na sio kuwatumikia wanachi kama inavyotakiwa.

Hivi karibuni Rais ameteua, ametengua na kubadilisha vituo vya kazi kwa wakuu wa wilaya mabalimbali na huku wengine wakibaki katika vituo vyao vya kazi wengine wakibadilishwa vituo ni 26% ya walioteuliwa hii ni idadi ndogo sana kuleta mabadiliko. Katika hali isiyo ya kawaida ambayo ina viashiria vya rushwa ya madaraka na upendeleo tumeona kuwa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) viongozi wake wote wamepewa vyeo hii ina maana gani kwa taasisi hiyo yenye watumishi wengi wa umma? Hii sio namna ya kudhohofisha juhudi ya kuwa na taasisi imara ili kuweka mwanya wa kusubiria teuzi? Kwamba viongozi watakao kuwa kwenye taasisi hiyo wakumbuke kwamba Rais anaangalia hiyo taasisi na ukiwa rafiki kwa serikali yake utapata uteuzi? Huu sio mgongano wa maslahi? , Katika teuzi hizi  Rais wa CWT  Leah Ulaya kateuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Makamu wa Rais wa CWT Dinah Mathani kateuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Uvinza na katibu wa chama hicho Bw Japhet Maganga ateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya Kyerwa, Hii inaibua swali kubwa sana kuhusu rushwa ya madaraka. 

  • Hii ina maana gani kwa viongozi wote wa ngazi za juu kuteuliwa kutoka kwenye chama hicho na kupata nafasi hizo?

Suala hilo la teuzi hizo za CWT halijatokea kwa bahati mbaya, Moja ya tuhuma ambazo Serikali ya CCM inazo kwa muda mrefu ni kudhibiti uchaguzi huru na wa haki, na kundi kubwa linalotumika kufanya hivyo ni kundi la walimu pamoja na Jeshi la Polisi na yeyote atakayeipa CCM ushindi mnono basi hulambishwa asali kwa kupewa madaraka na nafasi za uongozi, Lakini pia CWT ina idadi kubwa ya watumishi wa umma, wana suala mengi wanayoidai serikali, kukiwa na viongozi ambao wanasubiria teuzi inasaidia sana kupooza maslahi ya wanachama wa CWT, chama iki kinapodhohofisha watawala wanapata manufaa zaidi maana yanayozimwa ni maslahi ya walimu yaani kundi kubwa la watumishi wa umma, Serikali imefanya juhudi kubwa sana kuteka Taasisi za Dini, NGOs, na vyama vya siasa kupitia sheria mbalimbali, hata Tanganyika law Society ( TLS) na chama cha madaktari Tanzania , kinaongozwa na makada wa CCM

Huu umekuwa ni mtindo uliozoeleka wa kudhohofisha Taasisi ambazo zinasimamia maslahi ya wannachi wake, na serikali haina mpango wa kushughulikia changamoto zozote zile hivyo inachofanya ni kuvuruga wa uongozi wa hizo taasisi kwa kuweka mapandikizi kwenye hizo taasisi, lakini pia tunajua malalamiko mengi sana kuhusu BAKWATA sasa tunaona vyama vingine vinaingiliwa kwa kasi sana, hili la  sasa  Serikali ya chama tawala kutoa  vyeo kwa mtu ambaye ameshawahi kuvifanya kwa manufaa ya umma  kuendelea kuwepo madarakani,  Rais hateui viongozi hao kwa kuwa wana sifa na vigezo vya cheo husika. Kimsingi jambo hili ndio linachangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kukiweka chama tawala madarakani, hii ni mojawapo ya rushwa ambayo inaisumbua nchi kwa kuwa tunazidi kuwa na utawala mbovu kila kukicha.

Ili kuwe na utawala bora na kuepuka kadhia za utawala mbovu ulio na rushwa ndani yake ushiriki wa wananchi ni suala muhimu na la msingi sana katika kuchagua viongozi wao na  kujiletea maendeleo yao katika nchi. Mahali ambapo wananchi hawashiriki wala hawashirikishwi kunakuwa na lawama na mizozo mingi kwa viongozi hasa pale ambapo maamuzi yaliyopitishwa yanawaumiza wananchi ndipo tunaona umuhimu wa ukushiriki unajitokeza zaidi. Maamuzi yoyote ambayo serikali inayachukua yanatakiwa kuna msingi wa maoni ya wananchi.

Mwarobaini wa matatizo yote hayo ni #KatibaMpya ambayo itapunguza madaraka na mamlaka ya Rais na kuyaweka kwa wananchi ili viongozi wawe na maadili, wasiwe juu ya sheria na wawepo madarakani kwa ridhaa ya wananchi na kuwatumikia wananchi kwa utumishi uliotukuka kwa kuhofia uwajibishwaji.

#ChangeTanzania #WenyeNchiWananchi 



Leave a Reply